Mpaka upi utakaoniwezesha kufika Nairobi kwa kupitia Bunjumbura, Kigali na Kampala?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mwezi ujao ninatarajia kwenda Nairobi nchini Kenya. Kwa kuwa sijawahi fika Kigali, ninataka nitumie fursa hiyo kwa kupita kama njia.

Matamanio yangu ni kupitia Bunjumbura na Kigali ambako kwa kila jiji nitalala siku moja. Baada ya hapo, nitaendelea na safari hadi Nairobi kwa kupitia Kampala.

Nivukie mpaka upi ili niweze kupita kwenye hayo majiji mawili?
 
Mambo mengine unacheka tu.......kujionea limbukeni ya watanzania
 
Mkuu ungetaja safari yako inaanzia mkoa gani ingekuwa rahisi zaidi kukushauri.
Plan uliyoitaja itakulazimu kupiata border ya Manyovu/Mabanda ili kuipata Bujumbura au Gitega. Hiyo ni safari ya masaa kama 5-6. Kuingia Rwanda kutokea Burundi inawezekana lakini pitia mpaka wa Nyamata/ Bugesera au Rusumo.
Kutoka Kigali kuipata Kampala mpaka unaofahamika ni Gatuna kaskazini mwa Kigali. Kutoka Kampala utakuwa na chaguo kupitia mpaka wa Busia au Malaba. Lakini Malaba ndio border inayokufaa zaidi kama unaenda hadi Nairobi.
Kila la kheri mkuu!.
 
Mwezi ujao ninatarajia kwenda Nairobi nchini Kenya. Kwa kuwa sijawahi fika Kigali, ninataka nitumie fursa hiyo kwa kupita kama njia.

Matamanio yangu ni kupitia Bunjumbura na Kigali ambako kwa kila jiji nitalala siku moja. Baada ya hapo, nitaendelea na safari hadi Nairobi kwa kupitia Kampala.

Nivukie mpaka upi ili niweze kupita kwenye hayo majiji mawili?
Taifa linapitia kipindi kigumu sana🙏
 
Mkuu ungetaja safari yako inaanzia mkoa gani ingekuwa rahisi zaidi kukushauri.
Plan uliyoitaja itakulazimu kupiata border ya Manyovu/Mabanda ili kuipata Bujumbura au Gitega. Hiyo ni safari ya masaa kama 5-6. Kuingia Rwanda kutokea Burundi inawezekana lakini pitia mpaka wa Nyamata/ Bugesera au Rusumo.
Kutoka Kigali kuipata Kampala mpaka unaofahamika ni Gatuna kaskazini mwa Kigali. Kutoka Kampala utakuwa na chaguo kupitia mpaka wa Busia au Malaba. Lakini Malaba ndio border inayokufaa zaidi kama unaenda hadi Nairobi.
Kila la kheri mkuu!.
Nipo Mwanza mkuu
 
Kama uko Mwanza itakulazimu kuipita Kabanga/Kobero border, kutoka Kobero unaweza kuunganisha hadi Bujumbura siku hiyo hiyo masaa ni yale yale 5-6
Nashukuru sana mkuu. Nilikuwa nawaza hivyo ila sikuwa na uhakika kama nilikuwa sahihi. Nilitaka tu kujisahihisha kwa wazoefu.

Many thanks mkuu🙏🙏🙏
 
Mkuu ungetaja safari yako inaanzia mkoa gani ingekuwa rahisi zaidi kukushauri.
Plan uliyoitaja itakulazimu kupiata border ya Manyovu/Mabanda ili kuipata Bujumbura au Gitega. Hiyo ni safari ya masaa kama 5-6. Kuingia Rwanda kutokea Burundi inawezekana lakini pitia mpaka wa Nyamata/ Bugesera au Rusumo.
Kutoka Kigali kuipata Kampala mpaka unaofahamika ni Gatuna kaskazini mwa Kigali. Kutoka Kampala utakuwa na chaguo kupitia mpaka wa Busia au Malaba. Lakini Malaba ndio border inayokufaa zaidi kama unaenda hadi Nairobi.
Kila la kheri mkuu!.
Huyu nae,basi tu. Si angetaja hata anakotokea. Kama utatokea Kigoma, Manyovu/Mabanda ndo rahisi. Pitia Bujumbura, nenda mpaka Akanyaru. Kama upo karibu na Ngara,pitia Kabanga na Kobero, utakuja kutokezea Bugesera,unaingia Kigali. Njia nyingine, pitia Rusumo,nenda Kigali. Hope utakuwa unatalii. Au ukiwa Bujumbura,nenda Rusizi. Njia ni nyingi huwezi zitaja. Ila kwa ukaribu, Nyakanazi, Runzewe-Geita, Mwanza-Sirari,ni karibu.
 
Safari yangu ni ya Nairobi. Lakini kwa kuwa ninapenda "kutalii", nimeona nipite route ambayo sijawahi pita.

Ni kweli mkuu, kwa Mwanza mpaka wa Sirari ni karibu sana. Nauli ya Mwanza hadi Sirari ni shilingi elfu kumi tu, ilhali kutoka Mwanza hadi Ngara inaweza ikawa zaidi ya elfu ishirini.

Pamoja na kuwa gharama itaongezeka kidogo, lakini lengo langu litatimia.

Ninaua ndege wawili kwa jiwe moja: kufanikisha jambo linalonipeleka Nairobi na pia "kutalii" Bunjumbura na Kigali.
 
Ok. Safari yako,inaanzia wapi?
 
Mwanza mkuu.
Mi naona kama ni utalii, pitia Kigoma(Manyovu/Mabanda). Utashuhudia na urembo wa watoto wa Burundi. Hapo Mabanda kalikuwepo kadada,Alice,kazuri vibaya mno. Mengine hayakuhusu. Hahahahaha. Pitia Rumonge na Nyanza lake,furahia ulowe(ugali furani wa warundi). Fika mpaka Bujumbura,hapo ni kama siku mbili. Siku ya tatu,toka Bujumbura,pitia Gitega,pitia mpaka wa Mayange(Bugesera),upande wa Rwanda. Njia ya Akanyaru,haina mvuto. Siku hiyo hiyo,utalala Kigali. Kesho yake, panda gari ndogo tu(Rwanda ni Coaster),nenda Cyanika. Border ya Rwanda na Uganda. Hapo utatoka kuelekea Kampala. Njia ya kwenda Nairobi huko, mi niliishia Jinja,ukifika,rudi hapa utaelekezwa na wanaopajua.
 
Back
Top Bottom