Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Kutoka........
....mpaka.....
Neway ushauri wenyewe unasema hivi ''KAMA UNAWEZA KUMWONA HUYO ULIYENAE AKIKUFUNGIA VIFUNGO VYA BLAUZI UZEENI WAKATI WEWE HUWEZI TENA, BASI HUYO NDIE''.Kwahiyo kama unaweza kuona mkiwa pamoja miaka mingi baadae, wakati nguvu za kufanya mambo unayofanya mwenyewe huna tena na mwenzako akikusaidia basi ujue umempata mtu ambae anakufaa, moyo wako umemkubali.
That got me thinking, hivi ni wangapi waliopo kwenye uchumba na walioingia ndoani tayari wanafikiria hata kuwa pamoja na wenzi wao miaka minne mitatu mbele huku wakiwa na furaha? Hapo ulipo, unamwonaje mwenzi wako,Akizeeka, au hata akipata matatizo tu ambayo yatamfanya akutegemee wewe kwa kiasi kikubwa will you be there for him/her completely?No regrets or complaints? Utamsaidia kwa fahari? Au ndio utatamani Mungu amchukue mapema???
I hope the answers are YES, DEFINATELY, ABSOLUTLY NO REGRETS, YES and GOD NO!
Kama sio pole kwa kuwa kwenye ndoa na mtu ambae hajaziteka hisia zako kikamilifu. Naomba Mungu wale ambao bado wapo wapo siku wakiamua kuuga ukapera watatafuta watu ambao wanakubalika mioyon, nafsini na akilini mwao ili wimbi wa ndoa zinazovunjika ama zile zinazozaa manyanyaso/dharau/udanganyifu na mengineyo yapungue.