My Take:
Huu ndio Ubaya Ubwela wenyewe Sasa.πππππ
---
Your browser is not able to display this video.
Katika hali isiyo ya kawaida katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Edward Futakamba Mkazi wa Kata ya Nsemulwa amewashangaza wengi baada ya kufanya sherehe ya harusi licha ya Bibi harusi kugoma kufunga ndoa hiyo.
Edward aliyekuwa akiishi na Mwanamke aitwaye Marry na kufanikiwa kupata Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu ambapo baadae waliamua kwa pamoja kufunga ndoa na taratibu zikaendelea ikiwemo kutoa mahari ya shilingi 1,200,000/- na maandalizi ya harusi kufanyika ili ndoa ifungwe July 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya harusi hiyo Simon Moshi amesema siku nne kabla ya tarehe hiyo walipata taarifa kuwa upande wa Bibi harusi wameweka pingamizi kanisani la kuzuia ndoa hiyo βTulijaribu kuwatafuta kuongea nao ili angalau hili suala liende kama lilivyokuwa lakini ikashindikana, tukaona haiwezekani Watu wametoa mchango yao alafu hili suala likatishweβ
βSababu ambayo sisi tuliambiwa kama kamati walisema kwamba kwanza bwanaharusi alikuja amechangamka kwenye send off na wakasema kwamba kuna laki mbili haijamalizwa ya mahariβamesema Katibu wa Kamati ya harusi.
βKupata na kukosa yote ni sehemu ya maisha, cha msingi sana ikiwa kama Mtu unaweza kusherehekea na kufurahia ukipata basi ni vizuri pia hata ukikosa pia usherehekee na kufurahia kwa sababu mpango wa Mungu yeye ndio anayejuaβ amesema Edward Futakamba.
Mwisho
Unataka utaolewa ,hutaki utaolewa Kwa lazima πππ
Kuna makabila yana shida unakuta wanataka mahari yote ilipwe isibaki hata mia
Ila na mfungishaji wa hiyo ndoa hakuwa makini kama sababu ni hizo mbili za kuchangamka send off na kutomalizia mahari sio za msingi kama wao wawili wanaooana wamekubaliana
Angewaeleza hao wazazi walioweka pingamizi kuwa hiyo kikanisa sio pingamizi ya msingi inayoweza zuia ndoa kufungwa
Kawaida inatakiwa kiongozi wa dini aseme hivi kama kuna yeyote mwenye pingamizi la kisheria kama sheria za nchi zinavyosema kuhusu ndoa kufungwa alete hilo pingamizi la kisheria hapa
Kutomalizia mahari na kuchangamka sio mapingamizi ya kisheria
Waandishi wa habari fuatiliane mkahoji Bwana harusi,bibi harusi na wazazi na huyo aliyekuwa afungishe hiyo ndoa halafu muweke full story nini kilitokea hasa