Uchaguzi 2020 Mpangieni Lissu mavazi kipindi cha Kampeni

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,947
Reaction score
7,939
Muonekano wa mgombea una tija sana kwa wapiga kura. Mavazi ya aina Fulani yatavutia wapiga kura vijana pekee, mengine wazee ,mengine kina mama na Mavazi mengine kina baba.

Lissu Kama mgombea urais hapaswi kujiamulia kuvaa atakavyo. Kamati ya kampeni ijikite kumpangia mavazi yatakayo mletea mashabiki na wapiga kura wa jinsia zote na rika zote.

Kuna Mavazi mengine ukivaa wabibi na wababu wanakuona mkorofi au mgomvi.
Wapiga kura si wanachadema pekee kwaiyo sio lazima sana kwa mgombea kutinga makombati na makofia ya Chadema. Avae suti Safi Kama anazovaa kanisani au nguo nyingine Ila aepuke kuvaa nguo zinazoendana na harakati zaidi. Kofia nazo aangalie aina za kofia za kuvaa.

Nafahamu watu watasema cha muhimu Ni ujumbe lakini bado Mavazi yanasaidia au kuharibu.

Mpaka Sasa Lissu naongoza kwa mikutano inayohudhuriwa na wanaume wa umri wa Kati na vijana. Magufuli anaongoza kwa kina mama wa umri mkubwa na wa Kati na kinababa wazee.

Ni jukumu la kampeni meneja na kamati yake kuona namna ya kuvutia kina mama kwa hotuba zinazowagusa directly hata Mavazi. Kina mama na mababu ndio wapiga kura tusiwaamini Hawa vijana wanaoshangilia barabarani wengi hata kadi hawana.
 
Aisee! Basi wamekusikia bila shaka watalifanyia kazi.
 
Babuu hatuangalii mavazi tunaangalia utu na uzalendo aliokuwa nao
 
Kwahiyo Magufuli naye avae suti kama anavyokuwa ikulu au kanisani na aache kuvaa shati la kijani ambalo ndio sare ya chama?
Ilimradi vazi ni la heshima mbele ya jamii ya waliostaarabika,sioni tatizo lolote hapo!
 
....hii sio miss Tz na kama hiyo ni ishu basi muondonei Wema kuongea na wamama maana wengi wanaogopa kuona skeleton inatembea ...

QUOTE="Msulibasi, post: 36648440, member: 262436"]
Muonekano wa mgombea una tija sana kwa wapiga kura. Mavazi ya aina Fulani yatavutia wapiga kura vijana pekee, mengine wazee ,mengine kina mama na Mavazi mengine kina baba.

Lissu Kama mgombea urais hapaswi kujiamulia kuvaa atakavyo. Kamati ya kampeni ijikite kumpangia mavazi yatakayo mletea mashabiki na wapiga kura wa jinsia zote na rika zote.

Kuna Mavazi mengine ukivaa wabibi na wababu wanakuona mkorofi au mgomvi.
Wapiga kura si wanachadema pekee kwaiyo sio lazima sana kwa mgombea kutinga makombati na makofia ya Chadema. Avae suti Safi Kama anazovaa kanisani au nguo nyingine Ila aepuke kuvaa nguo zinazoendana na harakati zaidi. Kofia nazo aangalie aina za kofia za kuvaa.

Nafahamu watu watasema cha muhimu Ni ujumbe lakini bado Mavazi yanasaidia au kuharibu.

Mpaka Sasa Lissu naongoza kwa mikutano inayohudhuriwa na wanaume wa umri wa Kati na vijana. Magufuli anaongoza kwa kina mama wa umri mkubwa na wa Kati na kinababa wazee.

Ni jukumu la kampeni meneja na kamati yake kuona namna ya kuvutia kina mama kwa hotuba zinazowagusa directly hata Mavazi. Kina mama na mababu ndio wapiga kura tusiwaamini Hawa vijana wanaoshangilia barabarani wengi hata kadi hawana.
[/QUOTE]
 
Wacha aendelee CCM tulishawaambia wana CCM wetu kuwa kuna watu watakuja kuhutubia wanavaa nguo za kijeshi la mgambo ni jeshi la waasi Waliofukuzwa jeshini kwa utovu wa nidhamu wakaunda chama chao kinaitwa Chadema wana mgombea uraisi anayevaa nguo za mgambo aliyefukuzwa jeshini kwa uzinzi na kubaka
 
Babuu hatuangalii mavazi tunaangalia utu na uzalendo aliokuwa nao
Ni kweli na nimeeleza hapo Ila appearance inaleta tafsiri kadha wa kadha. Wapiga kura ni watu wa makundi tofauti , kielimu historia umri tamaduni nk .

Si Kila mpiga kura aliwahi kumuona Lissu iwe kwenye mtandao au ana kwa ana. Wapo ambao kipindi hiki ndio wameanza kumuona(najua utakataa) na wake waliomfahamu sasa wanamtazama more critically.
 
Sasa mtu anajua hawezi kupata hata kura laki mbili mnampangi mavazi ya nini? Ameamua kukaa majukwaani ili kutoa matusi na kebehi kwa watanzania huku akiwa na hasira, maana bado anahasira juu ya kilichomkuta.
 
una uhakika haukupotea njia labda ulikuwa unakwenda kwenye show ya Bonge Fleva au Mkutano wa Bongo Movie?
 
Hawa ndugu zangu falsafa yao ni kutobadilika. Lissu na Magufuli kuna togauti moja au mbili kubwa. Magufuli tayari amekuwa rais na Lissu ndio anautolea macho urais. Magufuli anaweza kuvaa jikofia la Marlboro na isilete shida lakini kwa Lisu ikamfikirisha mpiga kura.

Hoja za wataleta vita hoja za wahuni tu hawa, hoja za watauza nchi zinaingia hapo.

Bado kuna sababu Chadema kutazama mavazi ya wagombea, Ikiwezekana kugharamia . Ni swala la kucheza na Psychology ya wapiga kura.

Magufuli si mjinga anaposema wachadema nipigieni kura wa CUF wa ACT nk . CCM ilifika pahala 2015 wakaiga M4C Chadema wakalalamika sana. Sasa CCM wanaiga sera au ahadi msifikiri wanafanya bila utafiti au ushauri wa wabobezi wa kampeni.

Hata ikibidi kuwavuruga CCM kwa kuvaa shati la kijani kwenye bàdhi ya maeneo avae atawavuruga sana. Kumbuka shati la kijani si kwa ajili ya chama Fulani tu.
 
Wanaojielewa hawafwati nguo .. Wanafwata sera .. Mbona nyerere alikuwa anavaa kaunda 98% bado akapigania uhuru na akaupata kiulaini ...
 
Wanaojielewa hawafwati nguo .. Wanafwata sera .. Mbona nyerere alikuwa anavaa kaunda 98% bado akapigania uhuru na akaupata kiulaini ...
Mwaka 2005 Rais mstaafu JK alipigiwa kura nyingi sababu kubwa muonekano.Kuna sababu nyingi kundi Fulani kupiga kura.

Subirini za wanaojielewa muone Kama hamjaandamana. CCM wanazipenda kura za wasiojielewa ambazo ni nyingi kupita hizo za wanaojielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…