Aristotle J8
Member
- May 29, 2021
- 77
- 95
Mpangilio wa vyeo vya JWTZ
May 16 2017 public
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) (Tanzania People’s Defense Force (TPDF)) ni jeshi lililoanzishwa mnamo mwezi Septemba katika mwaka 1964.
Lilichukua nafasi ya jeshi la Tanganyika Rifles lililorithiwa na ukoloni wa Kiingereza.
Hizi ni baadhi ya shughuli ambazo hufaywa na JWTZ
- Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
.- Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Kufanya mafunzo na mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote
.- Kufundisha umma shughuli za ulinzi wa Taifa.
Watu wengi hushindwa kuelewa mpangilio wa vyeo ndani ya jeshi hili na hivyo kushindwa kutambua alama fulani inawakilisha mwanajeshi mwenye cheo gani.
Hapa chini ni mpangilio wa vyeo vya JWTZ. Vyeo vyote vyote vya jeshi viko makundi matano , kila kundi lina maofisa wa ngazi tatu tatu isipokuwa kundi la juu wao wako ngazi nne, Vyeo vyao katika kila kundi vinapishana kwa ngazi moja moja.
Kundi la Juu ni la maofisa wa Juu, wanaitwa Staff Oficers ambalo ni la majeneali na wako wanne.
1. General (Jenerali) – Mkasi na nyota 4, pia gari yake ina nyota 4, anaitwa A Four-Star General.
2. Lieutenant General (Luteni Jenerali)- Mkasi na nyota 3, pia gari yake ina nyota 3, anaitwa A Three-Star General.
3. Major General (Meja Jenerali)- Mkasi na nyota 2, pia gari yake ina nyota 2, anaitwa A Two-Star General.
4. Brigadier General (Brigedia Jenerali)- Mkasi na nyota 1, pia gari yake ina nyota 1, anaitwa A One-Star General.
Kundi la Pili kutoka juu ni la maofisa wakuu, wanaitwa Senior Oficers ambalo wako watatu. 1. Colonel (Kanali)- Ngao na nyota mbili
2. Lieutenant Colonel (Luteni Kanali)- Ngao na nyota moja
3. Major (Meja)- Ngao
Kundi la tatu kutoka juu ni la maofisa wa chini, wanaitwa Junior Oficers ambalo wako watatu
1.Captain (Kapteni)- Nyota tatu
2.First Lieutenant (Luteni)- Nyota mbili
3.Second Lieutenant (Luteni Usu)- Nyota moja
Kundi la nne kutoka juu ni la askari ambao sio maofisa, wa juu, wanaitwa Senior NCOs (Non Commissioned Officers) ambalo wako watatu .
1.Warrant Officer Class I (Afisa Mteule Daraja la Kwanza)- Ngao mkononi kama saa.
2.Warrant Officer Class II (Afisa Mteule Daraja la Pili)- Mwenge mkononi kama saa.
3.Staff Sergeant (Sajinitaji)- Ngao na mbavu tatu.
Kundi la tano na la mwisho ni la askari ambao sio maofisa, wanaitwa Junior NCOs (Non Commissioned Officers) ambalo wako watatu
1.Sergeant (Sajenti)- Mbavu tatu
2.Corporal (Koplo)-Mbavu mbili.
3.Lance Corporal (Koplo Usu)- Mbavu moja
Credit: SWAHILI TIMES

- Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa
- Kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
- Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa