Mpangilio Wa Vyuo Kwa MD

mnyalukoloh

Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
74
Reaction score
31
Habari Wana Jamvi.

Naombeni Mnishauri Nipangeje kozi Zangu Ili Nifanikiwe Kuinasa Medicine.

Mpangilio Nilio Upanga Uko Kama Ifuatavyo

>Kairuki
>IMTU
>Kampala

UfaUlu Wangu Ni Division Three
Phy D, chem Na Bio C
Mwaka Jana

Karibu Mni Shauri Mdogo Wenu Vip Nipangilie Ili Nifanikiwe.

Ahsante Na Karibuni
 
Imtu sikilifungiwa kimeshafunguliwa?Kampala si hakija sajiliwa?
 
omba huko imtu na kairuki but vyengine ni majanga tuu maana huwez kupata hukoo
 
Matokeo ya zamani hayakua na s wala e ni ABCDF tu

Mkuu hapana, mfumo wa matokeo ya zamani wa Kidato cha sita ulikuwa una E na S. Ulikuwa ni A,B,C,D,E,S na F.
Ushauri wangu kwake, asichague kabisa Kampala na Imtu, vyuo hivyo kwa sasa vina mgogoro mkubwa sana na serikali na wanafunzi, mara kadhaa vimefungiwa na serikali na pia wahitimu wake wamekuwa wakati mwingi hawatambuliwi na waajiri hususani serikalini.

Namshauri afuate mtitiriko huu wa ubora katika kuchagua vyuo kwa kozi za MD
1/Muhimbili(MUHAS)
2/KCMC
3/Bugando
4/Kairuki
5/UDOM
6/St.Francis.
 
Muhimbili pagumu watakula kichwa, aende Kairuki kama anataka mjini au UDOM,
 
Jaribu na AJUCo Songea hawa wachukua hadi CBG.
 
Usiwe unabisha usichokijua.

Alama za zamani kidato cha sita
A=80-100,
B=75-79,
C=65-74,
D=55-64,
E=45-54,
S=40-44
F=0-39.

alama mpya za kidato cha nne na cha sita
A=75-100,
B+=60-74,
B=50-59,
C=40-49,
D=30-39,
E=20-29
F=0-19.
Kama D Ambayo kwa sasa ni 30-39 zamani ingelikua F.
C kwa grade za zamani angelikua na aidha s kwa maana kama matokeo yake yangeangukia 40~44 au E endapo matokeo angelipata 45~50 sasa ngoja nimpe ufaulu wa juu kwa maana kwamba hizo C alipata 45~50 ambayo zamani ni E kwahiyo phys F chem na bios E Ambapo angelikuwa division 3 point 17 huyu anafaa kuwa daktari kweli si anaweza pasua mgonjwa kichwa tumbo baadala ya mguu. Taaluma ya udaktari ni nyeti dogo nenda ualimu.
 

Mimi siku zote napendekeza
Mtu akifeli hesabu huyo mtu hapaswi soma somo lenye hesabu yeye akawe mwandishi wa habari kama hawezi atafute kingine chakufanya kwani si lazima kila mtu asome fani fulani. Hii ndio yasababisha utendaji kazi mbovu sana maana watu ni kama wamelazimisha soma kitu walichofeli huko mwanzo.
Hawa ndio wanaenda chuo wanafeli mwaka wa kwanza
 

hapo ni sawa kabisa ila kulingana na ufaulu wake ajeuze iyo list upside down ili aendane na competition
 

Ww jamaa unaonekana mbishi sana...sasa sikia ni hivi according to Tcu;
Zaman Sasa. Pts
A A 5
B B+ 4
C B 3
D C 2
E D 1
S E 0.5
F F 0
Yeye kakwambia kapata CCD ya Brn hajakwambia amepata sijui 60,50,40,30 wala nn,sasa uki compare na zamani unapata DDE....Ukibisha na hapa basi ww utakuwa Milembe na si Molembe tena.
 
Anachokuambia hutu tu C twa mtoa hoja kimsingi ni kwa hisani ya BRN. Lakini kihalisia ni E na S kwa mpangilio wa zamani. Kama ni udaktari ajaribu KIU na IMTU. Vyuo serious havitampokea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…