Mpango au mipango ndiyo kitu muhimu sana katika maisha

Mpango au mipango ndiyo kitu muhimu sana katika maisha

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Habari ya uzima,

Katika MAISHA kitu muhimu huwa ni mipango au mpango. Katika philosophy huwa tunasema kuwa "life go to the same direction you gotta go with it"

Maana yake maisha huwa ni yale yale tangia zamani au tangia kuwepo kwa binadamu. Ila nikufata njia sahihi za hayo maisha. Ila kilichobadilika ni vitu au vifaa vya nje ambavyo hutumika kuendeshea maisha.

lakini maisha yapo vilevile tangu zamani. Basi baada ya hayo naanza kuelezea kuwa mipango au mpango is key in life. Ukianza kwa kuangalia haya mambo ulipanga kuwa nayo.

Mke wako au mme wako
Kazi unayofanya
Aina ya familia unayomiliki.

Ukiangalia sehemu hizo muhimu ambazo binadamu hutumia zaidi ya robo tatu ya maisha yake ni sehemu ambazo huwa hatukai na kuziingiza katika mipango na ndio sehemu ambazo zinatuumiza Sana , kihisia , kiakili na kiuchumi.

Ukitazama watu wazamani babu zetu lifespan yao ilikuwa juu kuzidi sisi ambao tuna vitu vingi ambavyo vinarahisisha maisha.

Maana yake nini tunaishi bila kuwa na mipango hasa katika sehemu yetu muhimu ambayo tutatumia zaidi ya robo tatu ya maisha yetu.

Tumeoa na kuolewa na watu tusiwaopenda kisa tu tulivutiwa na vitu vyao (material things ) na wengine tulioa mionekano tu hivyo unaishi miaka mingi ukigombana na mwandani wako na furaha hakuna mwisho unakufa mapema life span yako inashuka.

Kazi tunazofanya - wengi tunafanya kazi ili kuyafikia mahitjai ya msingi na sio kwamba Kazi tunazipenda, hivyo MTU anaishi kwa majuto na lawama hana furaha na anachokifanya.

Familia tulizonazo - hapa wengi baada ya kushindwa kufanikiwa hubaki na tumaini la kujitazama kupitia watoto wako uliowazaa kuwa watatoboa maisha na kuwa watu wa maana na mwisho wengi tumepata watoto ambao ukijitazama wewe unajiona na nafuu kuliko wanao.

Hakuna kitu mzazi anaumia anapomuona mwanae anakuwa mlevi kupindukia, malaya, mchipuko, muhuni mzazi anaumia sana hata kama anapesa anabaki kuishi kwa sonona.

Mzazi taswira au picha huwa ipo kwa watoto aliowazaa.

Hitimisho: Neno mpango limebeba dhana nzima ya maisha hivyo mambo ambayo yatachukua sehemu kubwa ya maisha yako usiyafanye kwa kukurupuka jipe muda Sana.

Familia
Kazi
Kuoa/kuolewa.

MTU mwenye mipango mizuri anakuwa na momentum anaanza taratibu katika starting line Ila lazima atakuwa wakwanza katika finish line.
 
Screenshot_20240128-190922~2.jpg
 
"""Neno mpango limebeba dhana nzima ya maisha hivyo mambo ambayo yatachukua sehemu kubwa ya maisha yako usiyafanye kwa kukurupuka jipe muda Sana"""

Vijana wenzangu Never engaged in marriage in younger age you have to fight for your own... In order your child to be in safe place.
 
Kilichobadilika ni vifaa vya nje vya kuendeshea maisha lakini maisha yapo vilevile hii

nimeipata kabisa.

Mfano zamani zilitumika ngamia ila kwasasa ni magari
 
Nafikiri umeamua kutukumbusha kuhusu umuhimu wa kuwa na Mipango binafsi katika kufikia lengo ama ustawi wa maisha.

Ukishakuwa na malengo utaishi Kwa;
  • Kupunguza idadi ya wapenzi maana kadri unavyokuwa na wapenzi wengi utajiingiza kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi lakini pia utalinda Wallet yako
  • Utaishi Kwa kuepuka tabia hatarishi za Uvutaji holela wa Sigara/Shisha/Bangi pamoja na tabia hatarishi za Ulevi wa pombe kupindukia.
  • Utaishi Kwa kufanya servings pamoja na kuwekeza kwenye assets ambazo zitakuja kukusaidia kwenye umri wako wa Uzee
  • N.K
 
"""Neno mpango limebeba dhana nzima ya maisha hivyo mambo ambayo yatachukua sehemu kubwa ya maisha yako usiyafanye kwa kukurupuka jipe muda Sana"""

Vijana wenzangu Never engaged in marriage in younger age you have to fight for your own... In order your child to be in safe place.
Ungekuwa unaandika hivi Kila siku......tunaofatilia nyuzi zako tungekuwa mbali sana😁😁😁
Ila tuendelee na mishangazi
 
Ungekuwa unaandika hivi Kila siku......tunaofatilia nyuzi zako tungekuwa mbali sana😁😁😁
Ila tuendelee na mishangazi
😂😂😂😂😂 Daaah mkuu mi naandika mambo safi mbona ni vile tuu nikipata mtu wa kuchanganya medulla yangu huwa sieleweki....

Mpaka sasa sio WAVE sio PARTICLE...
😂😂😂😂😂🤛🤛🤛
 
🙏🙏🙏Nakubali mkuu......ukipunguza mishangazi utakuwa role model wangu
Astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah

Weee seriously kumbe nina mtu wa kunifata huku 😂😂😂😂😂 ngoja jibadilike sasa mkuu
 
Astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah astakafillah

Weee seriously kumbe nina mtu wa kunifata huku 😂😂😂😂😂 ngoja jibadilike sasa mkuu
🤣🤣🤣Tupo mkuu tunaokufata na taarifa zako za habari
 
Mmoja akasema ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa.

Fail to plan is to plan to fail
 
Back
Top Bottom