Mpango wa dunduliza wa NHIF haueleweki

Mpango wa dunduliza wa NHIF haueleweki

Konny Joseph

Senior Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
118
Reaction score
199
Habarini za kazi wana JF!

Nimejaribu kufuatilia utaratibu wa Dunduliza katika NHIF lakini naona kama mifumo haisomani:

  • Ukienda NHIF kwenyewe.wanakwambia utembelee tawi la NMB lililokaribu yako kwa jaili ya usajili.
  • Ukiemda NMB wanakwambia wao hawafanyi usajili huo bali ujisajili mwenyewe kupitia USSD.
  • Ukiingia kwenye hiyo USSD mfumo haukubali kabisa, nimeshajaribu kwa siku tofauti kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.
Sasa nashindwa kuelewa ikiwa huu mpango upo kweli ama ni siasa tu za kiserikali,mana kama upo mbona kama kuna danidani nyingi kila ninapofuatilia.

Labda wenye uelewa zaidi na hili naomba mtusaidie!!
 
Back
Top Bottom