Mpango wa elimu na ushauri wa afya kupitia simu yako

said rashid

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Posts
203
Reaction score
112
MPANGO WA ELIMU NA USHAURI WA AFYA KUPITIA SIMU YAKO


UTANGULIZI
MPANGO WA ELIMU NA USHAURI WA AFYA KUPITIA SIMU YAKO
ni mpango wa wataalam na washauri wa afya wa AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS (www.afyazaidi.org , Facebook : AFYA ZAIDI Consultants ) kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na kuwasaidia kuwa na afya njema siku zote popote walipo Tanzania. Mpango huu unalenga kutoa elimu na ushauri kila siku kwa watanzania popote walipo kwa njia za kuongea nao kupitia simu, ujumbe mfupi wa maandishi na barua pepe na kuwapa elimu na ushauri juu ya masuala mbalimbali yanayohusu afya kwa ujumla, magonjwa, dawa, vyakula, urembo na vipodozi.
Mpango huu ni kwa ajili ya watu wote waliopo sehemu yoyote ya Tanzania.
Lengo kuu ni kulinda na kusaidia afya ya jamii na maisha kwa ujumla.

MALENGO YA MPANGO HUU

Lengo kuu la mpango huu ni kulinda na kusaidia afya ya jamii na maisha kwa ujumla.

Watu wote watajua vizuri kuhusu afya na kupata huduma za elimu na ushauri wa afya hata kama wapo mbali na hospitali.

Watu wote watakaojiunga na mpango huu watakuwa na wataalam na washauri binafsi wa afya na kupewa elimu na ushauri wa afya kila siku kuhusu afya kwa ujumla, magonjwa, vyakula, dawa, urembo na vipodozi.

Mpango huu unalenga kuwasaidia watanzania kuwa na upeo mpana zaidi wa afya zao na mambo yanayoathiri afya zao hivyo kuwawezesha kujilinda na kutunza afya zao

Mpango unalenga kusaidia watu kuwa na afya njema na amani kila siku ili kuweza kuishi vizuri na kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzalisha mali

Kwa wagonjwa, mpango huu unalenga kuwafundisha jinsi ya kudhibiti magonjwa waliyonayo na kuzuia matatizo yanayoweza kuwakabili wakati wanaendelea na matibabu

Mpango huu unalenga kusaidia watu kujikinga dhidi ya magonjwa na matatizo mengine ya kiafya

Pia mpango unalenga kuwapa watu wote uelewa wa dawa zetu na jinsi ya kuzitumia vizuri na kuzitunza ili zifanye kazi zake vizuri na kuwa na ufanisi mkubwa kila siku

Mpango unalenga kuwasaidia watu wote kuelewa vizuri vyakula, lishe na ulaji bora ili kuweza kupata matokeo mazuri kutokana na ulaji wetu bila kuathiriwa na matatizo mbalimbali yanayotokana na ulaji mbaya na lishe duni

Kwa upande wa urembo na vipodozi, mpango una lengo la kuwasaidia watu wote kuwa nadhifu na wanaopendeza kila siku. Unasaidia watu kuvijua vipodozi vyao kwa uzuri kabisa, kuvijua vipodozi vilivyo salama na visivyo salama na kuwaepusha dhidi ya madhara yote ya vipodozi visivyo salama. Pia watumiaji wote watajua jinsi ya kuwa na uzuri wanaoutaka, vipodozi vinavyoendana na miili yao, jinsi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali kama vile chunusi, mba, upele, makovu, harufu mbaya, michirizi, makunyanzi na kadhalika

Pia mpango unalenga kuwapa watu elimu ya huduma ya kwanza ili kuweza kukabiliana na ajali na matatizo mbalimbali ya kiafya kabla ya kwenda hospitali




JINSI MPANGO HUU UNAVYOFANYA KAZI

Mpango wa elimu na ushauri wa afya kupitia simu yako unafanya kazi kwa kukupigia simu, kukutumia meseji na kukutumia barua pepe mbalimbali zitakazo kupa elimu na ushauri juu ya afya yako kwa ujumla, magonjwa, vyakula, dawa, urembo na vipodozi. Pia utapewa namba za simu za wataalam wa afya na washauri wako binafsi ambazo utakuwa unapiga au kutuma meseji utakapohitaji elimu au ushauri juu ya suala fulani lihusulo afya yako kwa ujumla, magonjwa, dawa, vyakula, urembo au vipodozi.

Hivyo utakuwa unapata elimu na ushauri wa afya haraka zaidi na mara kwa mara kutoka AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS na utakuwa na washauri wako binafsi wa afya ambao watakuhudumia muda wowote utakapohitaji ukiwa sehemu yoyote.

JINSI YA KUJIUNGA NA MPANGO HUU

Kujiunga na mpango huu ni rahisi. Unaweza kujiunga kwa njia moja kati ya hizi zifuatazo:

1. Kufika ofisi za AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS zilizopo Temeke Buza (Mtaa wa Mashine ya maji No. 5), Dar es salaam na kujaza fomu ya kujiunga

2. Kutupigia simu AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS kupitia namba 0 659 528 724 au 0 784 082 847 au 0 718 717 801 au 0 785 856 680 kisha utasajiliwa na kupewa huduma

3. Kuwasiliana nasi kwa njia ya baruapepe kupitia anuani yetu ya info@afyazaidi.org na kisha utasajiliwa na kupewa huduma

Ada ya usajili ni shillingi elfu mbili tu (2,000/=) na baada ya hapo utapata elimu na ushauri wa afya, magonjwa, vyakula, dawa, urembo na vipodozi bure kwa muda wa mwezi mzima

JIUNGE SASA

Jiunge sasa na uanze kupata elimu na ushauri wa afya kila siku, wakati wowote na mahali popote ulipo.

Pia unaweza kumuunganisha ndugu, jamaa au rafiki ili aweze kupata elimu na ushauri wa afya kila siku, wakati wowote na mahali popote alipo.

Ili kusaidia watu wengi zaidi tafadhali wajulishe na watu wengine.

AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS TUNAKUTAKIA AFYA NJEMA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…