Mpango wa kuishitaki TANESCO na kampuni ya tiGO Tanzania

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2007
Posts
848
Reaction score
191
Mimi pamoja na mwanasheria wangu niko katika mpango wa kuandaa mashtaka kwa kampuni 02 hapa nchini TZ; na kampuni hizo ni TANESCO na TIGO Tanzania kwa huduma duni/dhaifu na zisizo thamini thamani ya fedha inayolipwa na wateja wake nchini kote.Hii ni katika kulinda haki za wateja kama wao wanavyolinda mali zao.

Hivyo basi, kama hizi kampuni zinanakukera kutokana na utendaji wake wa kazi za kila siku katika kukuhudumia ili kukuza uchumi wa mtu/watu na Taifa kwa ujumla.

Kwa maana hiyo wale wote watakaokuwa tayari kuungana na mimi kusaini hii petition; wathibitishe kwa mawasiliano zaidi:

kiuyajibu@jamiiforums.com/kiuyajibu@facebook.com

Siku zote"umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu"
 

kweli kuna kero sana hasa tanesco afadhali kidogooo tigo. Maana tanesco kila siku wanatukatia umeme tena sio kwa nusu saa ni masaa kwa siku
mimi nakuunga mkono
 
kwa tanzania utakuwa unajisumbua tu na wazo uache ilo suala utapoteza muda wako bure,nchi hii inakulindana na viongoz wana hisa kwenye hizo kampun,hivo acha wafu wazikane wenyewe utapoteza muda wako bure,utakuwa ni upepo wa kupita,wala ayatoshugulikiwa
 
Nafikiria kuongeza pressure hadi kwa nchi wahisani ili watuunge mkono katika vita kama hizi hadi zishughulikiwe;tutaomba misaada isitishwe mpaka hali kama hii ipate suluhisho.Lakini pia kwenye sehemu nyingine ambazo nikichocheo cha kukuza uchumi kama kuna uzembe tutaendelea kuomba wabane msaada ili akili zikae sawa.
Hii style pia inaweza kuifanya serikali kuwa makini/serious katika masuala ya msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…