Mpango wa kupiga marufuku matumizi ya petrol na dizel unaandaliwa na nchi zilizoendelea. Tuwe makini na miradi katika nishati hizi

Mpango wa kupiga marufuku matumizi ya petrol na dizel unaandaliwa na nchi zilizoendelea. Tuwe makini na miradi katika nishati hizi

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Niliwahi kutahadharisha miaka takriban minne iliyopita kuwa, siku za petrol and dizel zinakwisha na hivyo tufikirie vizuri zaidi kuhusu miradi mikubwa ya petrol and dizel. Nililenga moja kwa moja mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.

Technologia inabadilika kwa kasi sana siku hizi kuliko wakati wowote katika historia ya wanadamu. Huwezi kuamini kuwa technologia ya magari ya kuchaji na betri zake magari ambayo yapo mengi nchi za Ulaya, Amerika na Asia, technologia hiyo imeshaanza kufikiriwa kuwekwa pembeni ikiwa ni chini ya miaka 10 tangu mauzo makubwa ya kwanza kufanyika, na badala yake technologia ya matumizi ya engine za hydrogen inakuwa kwa kasi sana na inakwenda kuwa mbadala wa dizel na petrol.

Baadhi ya nchi za Ulaya tayari zimeweka mipango mikakati ya kuondokana na matumizi ya mafuta ifikapo 2035 (miaka 10 ijayo)! Kati ya nchi hizo ni Norway ambayo zaidi ya 50% ya magari yao ni ya umeme!

Wakati wenzetu walioendelea wanaondokana na matumizi ya mafuta yanayochafua mazingira, sisi Afrika tunaonekana kutoamini kuwa siku za petroli na dizeli zimekwisha. Kuna uwezekano mkubwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania utakuwa white elephant. Tuwe makini na tusome alama za nyakati la sivyo tutapata hasara kubwa kwa kutumia vibaya mikopo yetu!

Ni leo tu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza upigaji marufuku wa mafuta ya mwambani (fossil fuels) ili kuokoa dunia kutokana na uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa. Soma zaidi hapa: Climate change: Ban fossil fuel advertising says UN chief
 
Hata

Hata huko anapopasema badoooo sana. Labda tuliokuwepo duniani jumlisha watakaokuja miaka 100 ijayo wote tufe.
Na sitashangaa kusikia Tanzania imegundua Gari linalotumia Nishati ya Mkaa.
 
Back
Top Bottom