Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Mwaka 2020 ndo huu hapa.
Achana na ya 2019. Umepiga hatua kubwa sana mpaka kufikia siku ya leo ukiwa mwenye siha njema. Kama umefanikiwa kuuona mwaka mpya basi ujue kwamba ulifanikiwa kula vizuri, kulala vizuri na kuwa nafuraha ndio maana umefika leo.
Hapa sasa nataka tuzungumzie kuhusu 2020 na mafanikio yako,SIKU KWA SIKU.
Ili kufikia malengo yako kwa mwaka 2020 tafadhali weka maisha yako katika makundi matatu:
Katika Uchumi na Biashara weka malengo kama haya,

- Maisha ya Kibiashara na Kiuchumi
- Maisha ya binafsi,kimahusiano na Kifamilia
- Maisha ya kijamii kwa ujumla wake
Katika Uchumi na Biashara weka malengo kama haya,
- Kuweka AKIBA ya angalau 10% ya pato lako la siku
- Kuwekeza angalau 10% ya pato lako
- Kutengeneza mtandao wako wa WATEJA,WABIA,SUPPLIERS angalau MMOJA KWA WIKI
- KUWEKA MIPNGO YA KIBIASHARA ya MUDA MFUPI,WA KATI na MREFU
- KUJIFUNZA UJUZI MPYA UNAOWEZA KUKUONGEZEA UFANISI,KIPATO au FURSA
- KUACHA KABISA TABIA YA KUAHIRISHA MAMBO
- KUACHA KABISA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI PESA NA RASILIMALI MUDA
- Kuongeza ukweli na uwazi katika mawasiliano ya kifamilia
- Kutoa na kupokea ushauri bila kinyongo
- Kujipatia ME time angalau mara moja kwa mwezi
- Kutenga FAMILY time angalau mara moja kwa mwezi
- Kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wako
- Kufanya Ibada za pamoja katika Familia
- Kushiriki katika shughuli za kijamii zenye TIJA kama vile usafi wa mazingira au volunteer activities katika eneo lako
- Kupanda Angalau Mti Mmoja wa Matunda
- Kufahamiana na Majirani zako kwa kuwatembelea au kuwaalika kwa chakula cha jioni au hata kupata kinywaji,
- Kusikiliza na kuwashauri wale wanaohitaji msaada wako,Wape wote connection nao watakupa connection