Mpango wa Mafanikio mwaka 2020-Kijasiriamali zaidi

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Mwaka 2020 ndo huu hapa.

Achana na ya 2019. Umepiga hatua kubwa sana mpaka kufikia siku ya leo ukiwa mwenye siha njema. Kama umefanikiwa kuuona mwaka mpya basi ujue kwamba ulifanikiwa kula vizuri, kulala vizuri na kuwa nafuraha ndio maana umefika leo.

Hapa sasa nataka tuzungumzie kuhusu 2020 na mafanikio yako,SIKU KWA SIKU.

Ili kufikia malengo yako kwa mwaka 2020 tafadhali weka maisha yako katika makundi matatu:

  1. Maisha ya Kibiashara na Kiuchumi
  2. Maisha ya binafsi,kimahusiano na Kifamilia
  3. Maisha ya kijamii kwa ujumla wake
Kumbuka katika haya makundi matatu ndiko maisha yetu wote yana base na uwezo wa kuweza kuwa na balance katika maeneo haya yote ndo utaamua iwapo utakuwa na mafanikio na furaha au la.Usikubali eneo moja liathiri eneo lingine.LIVE a BALANCED LIFE.

Katika Uchumi na Biashara weka malengo kama haya,
  1. Kuweka AKIBA ya angalau 10% ya pato lako la siku
  2. Kuwekeza angalau 10% ya pato lako
  3. Kutengeneza mtandao wako wa WATEJA,WABIA,SUPPLIERS angalau MMOJA KWA WIKI
  4. KUWEKA MIPNGO YA KIBIASHARA ya MUDA MFUPI,WA KATI na MREFU
  5. KUJIFUNZA UJUZI MPYA UNAOWEZA KUKUONGEZEA UFANISI,KIPATO au FURSA
  6. KUACHA KABISA TABIA YA KUAHIRISHA MAMBO
  7. KUACHA KABISA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI PESA NA RASILIMALI MUDA
Katika Maisha Binafsi,Mahusiano na Familia weka malengo kama haya;
  1. Kuongeza ukweli na uwazi katika mawasiliano ya kifamilia
  2. Kutoa na kupokea ushauri bila kinyongo
  3. Kujipatia ME time angalau mara moja kwa mwezi
  4. Kutenga FAMILY time angalau mara moja kwa mwezi
  5. Kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wako
  6. Kufanya Ibada za pamoja katika Familia
Katika Maisha ya Kijamii kwa ujumla wake;
  1. Kushiriki katika shughuli za kijamii zenye TIJA kama vile usafi wa mazingira au volunteer activities katika eneo lako
  2. Kupanda Angalau Mti Mmoja wa Matunda
  3. Kufahamiana na Majirani zako kwa kuwatembelea au kuwaalika kwa chakula cha jioni au hata kupata kinywaji,
  4. Kusikiliza na kuwashauri wale wanaohitaji msaada wako,Wape wote connection nao watakupa connection
 
Asante na umeeleweka vyema kabisa.
 
Mwaka ujao tusiulizane UNA NYUMBA, UNA GARI? Tuulizane una biashara gani? Unaongeza mradi gani? Unatumia mbinu gani kuuza bidhaa zako n.k
 
Safi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…