Mpango wa serikali ya Tanzania kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanaume wa Dar

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Habari wana jf!!

Nimatumaini yangu kuwa wote ni wazima wa afya.
Leo ningependa tuzungumzee juu ya mpango endelevu wa serikali ya Tanzania katika kutatua suala zima la ukosefu wa ajira nchini (betting),mpango huu endelevu uliletwa na serikali kwa dhumuni la kuwakwamua wanaume wa Dar pamoja na divisheni zero zilizo jaa hapa nchini kila kona.

Inasemekana kutokana na serikali kutambua uvivu na usharobaro wa wanaume wa Dar kwa kupitia matukio mbalimbali kama:

1.kujificha chini ya magari wanaposkia tetesi za panya road kuwa wamefika katika eneo lao wakati panya road ni vijana wadogo wanaokadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 15-19.

2.Mtu mmoja 'scorpion' kutishia buguruni nzima

3.Vijana kupenda kuwa 'marioo'

Hivyo,serikali ikapitisha mpango huu ambao sasa unaonyesha matunda kwa kuwa vijana wengi wamejikitaa katika swala zima la kubeti hivyo kusababisha kelele za ukosefu wa ajira kupungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.
 
Hivi kwanini sisi wanaume shupavu wa Dar mnatuchanganya na hao wa mikoni wanaofanya hayo uliyoyaandika? Wanaume wa Dar huwa hatufanyi yote hayo
 
Hivi kwanini sisi wanaume shupavu wa Dar mnatuchanganya na hao wa mikoni wanaofanya hayo uliyoyaandika? Wanaume wa Dar huwa hatufanyi yote hayo
Wanaume wa Dar mnamatatizo kwa kweli,tunawaomba mjirekebishe.
 
Hivi kwanini sisi wanaume shupavu wa Dar mnatuchanganya na hao wa mikoni wanaofanya hayo uliyoyaandika? Wanaume wa Dar huwa hatufanyi yote hayo
ila wanaume wa dar wamezidi wanakimbia hadi end product zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…