Mpare Na Pesa Benki

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
11,605
Reaction score
1,843
Kuna Mpare mmoja anaishi karibu na Benki, baada ya kushawishiwa kwa muda mrefu na ndugu na marafiki zake aweke pesa Benki kwa usalama wa pesa zake, kwa taabu sana akakubali kuweka pesa Benki. Kuanzia siku hiyo alizoweka hizo pesa, usiku kucha anakesha dirishani na filimbi mdomoni, kila akipita mtu karibu na hiyo Benki, Mpare wa watu anapiga filimbi kuwaamsha walinzi piii... piiiii....! Wote woga anaogopa, asije mtu akaiba pesa zake....!
 
duh!
Unamaanisha mchaga??????
Ukiongelea mabo ya malavidavi au ubahili ndio utaje wapare...na kwenye mambo ya kibeeenki wataje kina massawe
 
duh!
Unamaanisha mchaga??????
Ukiongelea mabo ya malavidavi au ubahili ndio utaje wapare...na kwenye mambo ya kibeeenki wataje kina massawe
Kaka Issue imemtokea mzee wa Kipare!
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa iyo kali
 
mpare na msambaa hawana tofauti
sema wapare wanapenda sana kesi, kesi na kuku anaweza akauza kiwanja ili amlipe wakili
Eeeh! Kumbe, nilikuwa sifahamu ilo mkuu!
 
mpare na msambaa hawana tofauti
sema wapare wanapenda sana kesi, kesi na kuku anaweza akauza kiwanja ili amlipe wakili
Ndio maana mzee wa Kipare anakesha akilinda Benki!
 
mpare na msambaa hawana tofauti
sema wapare wanapenda sana kesi, kesi na kuku anaweza akauza kiwanja ili amlipe wakili

Aisee! hii ni kweli nimeyaona kwa majirani zangu hao wapare!! hehehehe! wanapenda kesi hao! duuhhhh!!hehehehehehh
 
Jamani wadau wangu mbona mnatuonea sie akina NITHITHI THITHI BABA ZAO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…