Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Ndugu wanajamiiforum hii leo kupitia channel ten niliona vyama vya upinzani wanalalama kuhusu mchakato mzima wa kuipata katiba mpya. Mimi kama mwanasheria mchanga kabisa, naona dalili za katiba yenye malalamiko ambayo haita dumu, kwani katiba ni kama msingi wa nyumba sasa kama msingi wa nyumba unanyufa kabla nyumba haijaisha, nimpumbavu pekee atake kaaa kwenye nyumba hiyo, kwani si muda mrefu tu itabomoka. Kila mtanzania aridhike na mchakato mzima, la sivyo tuisusie huu mchakato kwasababu hata kama sisi tunaridhika kama hao wapinzani hawalidhiki nchi itasambalatika sasa naomba wanaCCM wenzangu tuwaridhishe hawa wapinzani tusiwadharau. Tukiwadharau wakawa maadui wakaungana na maadui wa taifa hili(kutoka nje) habaki mtu!