BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Maafisa wa upelelezi katika Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walilazimika kumfungulia mashtaka Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhusiana na kesi ya ufisadi wa Tsh. Bilioni 140.3, afisa mkuu wa polisi amefichua.
Pia imeelezwa wakati wa kumkamata Gachagua na kufikishwa kortini Julai 26, 2021, uchunguzi ulikuwa haujakamilika na hakukuwa na ushahidi wa maandishi kuunga mkono makosa hayo.
Wakati huo Naibu Rais Gachagua alikuwa Mbunge wa Mathira.
Katika hati ya kiapo iliyosainiwa na msimamizi mkuu wa polisi Kuriah Obadiah, ambaye yuko katika makao makuu ya DCI, alisema maafisa walisukumwa kumkamata na kumshtaki Bw Gachagua kwa uhalifu wa kifedha.
Bw Obadiah, ambaye ni mkuu wa kitengo cha Uhalifu Mkubwa, alikuwa kiongozi wa timu ya uchunguzi iliyoundwa kumsaka mwanasiasa huyo, ambaye alitofautiana na utawala wa Rais wa zamani Uhuru Kenyatta.
Akieleza kuwa alishinikizwa sana na aliyekuwa mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, George Kinoti ili kutoa mapendekezo ambayo yangempeleka Gachagua kizimbani, afisa huyo aliongeza kuwa alipewa muda maalum kuhakikisha hilo linafanyika.
"Mnamo Aprili 15, 2020, DCI ilipokea barua kutoka Kituo cha Kuripoti Fedha ikitoa madai ya uhalifu dhidi ya washtakiwa wanaodaiwa kuhusika na ubadhirifu wa pesa kutoka Bodi ya Taifa ya Umwagiliaji na mashirika mengine," Anasimulia Obadiah katika hati ya kiapo ya kurasa nne.
==================
The report, he says, was transmitted to his section at DCI with clear instructions to promptly carry out investigations including recording of statements, searches, and filing of affidavits in court for orders to access the accused persons’ bank accounts, among other activities.
“The investigations team headed by myself was given strict and fixed timelines to come up with findings promptly which made it difficult to conduct thorough and comprehensive investigations into the allegations,” states Mr Obadiah.
He goes on to state that “while the investigations were still in progress, Mr Kinoti directed us to make recommendations that will enable the accused persons to face charges”.
After being arraigned in court, the detectives abandoned the investigations.
They raised six allegations related to fraud, money laundering, abuse of office and conflict of interest. The trial never moved to hear witness testimony.
The case is set to come up on November 21, 2022, for directions on the withdrawal.
Mr Gachagua is also at the Court of Appeal fighting forfeiture of his Sh200 million that is alleged to be unexplained wealth.
NATION MEDIA