Mpemba na kioo cha Kijapani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Japan Airport wameweka kioo kubwa ukisimama mbele yake inataja jina lako na nchi unayo elekea.

Mpemba mmoja alisimama mbele ya kioo akaambiwa jina lake ni Awadhi Mkufu Mbaruku na ndege yake yaelekea Zanzibar.

Awadhi alishangaa na kioo na akataka kuhakikisha kuwa ni kweli. Akaenda kuvua koti akavaa kanzu, kofia na miwani. Akarudi tena mbele ya kioo na akaambiwa tena kuwa jina lake ni Awadhi Mkufu Mbaruku na ndege yake yaelekea Zanzibar.

Awadhi akaenda tena kuvua kanzu zawadi alizokuwa amemnunulia mkewe. Akavaa night dress, akatia rangi ya mdomo na akatafuna ubani na kulegeze mwili. Akarudi tena kwenye hicho kioo na akaambiwa

"Jina lako Awadhi Mkufu Mbaruku na ndege yako ishakuacha kwa ukhanithi wako!"
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23]
 
Hahahahaha nooma sana na uhanisi wake[emoji23][emoji23]
 
Do Mpemba noma.
 
Yakhee watuzulia wapemba hatunaga hayo mambo labda wale wenzetu wa kondoa[emoji18] [emoji12] [emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…