Mpemba

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
6,829
Reaction score
1,303
Jamaa mmoja wa kipemba aliyekuwa hajawahi kupanda gari hata siku moja,
alikuwa anasafiri kwenye basi akiwa kwenye siti ya mbele kabisa.
Mara ikatokea ajali na baada ya tukio hilo la ajali yule jamaa
akatakiwa kutoa ushahidi mahakamani na ushahidi wake ulikuwa kama
ifuatavyo;


"kwanza wakati safari yaanza tu nkajua kuwa huyu si dereva! kuna
lijiti akikazana kuling'oaaa"(wakati dereva akiingiza gia),
"halafu akawa hatulii mikono ikintetema"(akizungusha msukani).
"Njiani ikawa ni mbio tu! twafukuzana na miti,miti yenda na sie
twenda,nliposikia puuu! nkajua tayari ivooo! miti ishatugonga au sie
tushaigonga miti
 
ha ha ha!! yawezekana ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda gari huyu Mpemba.
 
Aaaaaaaaa Mpembaaaaaaaa!!!!!!!!!!
Kunamwengine mkewe alimegwa akamwambia we endelea na nchezo wako na mi ntatoa kwa back ntaa nzima ili nkutie aibu
 
Wewe Masikini jeuri usitafute vita na wapemba na kwa taarifa yako
wenyewe wapo na bado ni imara, na isiwe wewe mwenzetu ni kutoka Kae
 
Wewe Masikini jeuri usitafute vita na wapemba na kwa taarifa yako
wenyewe wapo na bado ni imara, na isiwe wewe mwenzetu ni kutoka Kae


Just joke Mkuu Sultan; c wajua Wabongo sie udugu wetu unajengwa na kutaniana pia? :becky:
 
Wapemba twataniwa sana wallah.
Hivi nyie mijitu ya bara mwadhani Pemba ni punda tu ziko?
Hata Chai maharagwe zipo kwa wingi.
 
eee baba tusipopoteza wakati kwa kutaniana basi mambo
hayatakua mazuri. basi lakini mimi nilisikia kua kisa hichi kilitokea unguja
gari likitokea kae kuelekea mjini , na huyo jamaa ni mmakunduchi
basi sijui ipi ni kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…