Kuna msemo unasema ' To love is nothing, to be loved is something, to love and to be loved is everything' Ndio maana nimesema mpende akupendae Mapenzi ni kitu cha muhimu sana katika maisha ili uwe na maisha ya furaha siku zote lazima uwe na mapenzi kweli, hizi kesi za Baba katembea na housegirl, mama haouseboy, small house n k. Hazitakuwepo kama tukiwa na mapenzi ya kweli Trust in God, mchana mwema wa JF na mlo mwema ni hayo tu kwa leo.
NIMEUKUTA KULEEEE GLOBAL PUBLISHERS
"Yule jamaa anayejiita Nabii Tito ameibuka na kioja cha kufungulia mwaka 2011, Risasi Mchanganyiko linaweka mambo hadharani.
Tito anayehubiri imani yenye ukakasi katika baa mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni ametoa kijarida (Risasi Mchanganyiko lina nakala) kinachoeleza kuwa ni ruksa kwa akina baba ambao ni waumini wa mahubiri yake ‘kulala' na wafanyakazi wao wa ndani (mahausigeli).
Katika nukuu za kijarida hicho, Tito anatoa mfano kutoka Kitabu cha Mwanzo cha Biblia kuwa, Mtumishi wa Mungu Abraham alizaa mtoto wa kiume, Ishimaeli (Ismail) na kijakazi wake Ajili.
Aidha, katika kijarida hicho, Tito anasema kuwa akina baba kuwaacha mahausigeli wao ni dhambi mbele za Mungu na kusisitiza kwamba, lazima wapewe haki yao kama alivyofanya Abraham.
Kwa mujibu wa watu waliokisoma kijarida hicho anachouza shilingi za Kitanzania 1,000, wamemponda Tito kwa mahubiri hayo kuwa ni ya upotoshaji huku wakitoa tahadhari kwamba akiachwa, anaweza kuiharibu nchi.
Mwaka jana, Tito aliripotiwa na gazeti hili kutoa kijarida kingine kinachoruhusu watu kunywa pombe na wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja.
Habari hiyo ilieleza kwamba, mahubiri hayo yalilaaniwa vikali na watu wanaomwamini Mungu ambapo gazeti hili lilikipeleka kijarida hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar (wakati huo), William Lukuvi ambaye aliagiza kukamatwa mara moja kwa mtu huyo.
Cha kushangaza mtu huyo hakukamatwa na badala yake anapeta kwenye mabaa akieneza mahubiri hayo yanayolaaniwa kila kukicha na viongozi wa dini."