Mpende mkeo kwa mitindo

Mpende mkeo kwa mitindo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kama kuna kitu kimetushinda wababa wengi ni kujua mkeo anataka nini hasa kwenye ishu nzima ya mitindo ya nywele za kusuka, hebu pata darasa la bure hapa mitindo michache ili usibabaike shemeji akikwambia;
.. Majongoo makubwa
.. Majongoo madogo
.. Mtindo huu umechukua shepu ya mdudu jongoo
.. Yebo Yebo kubwa
.. Yebo Yebo ndogo
.. Msuko huu asili yake ni Africa kusini
.. Mkonga wa jogoo, unafanana copyright na shungi la jogoo
.. Sangita ndogo
.. Sangita kubwa
Hizi wataalam wake ni wamasai no mtindo ghali lakini wenye kupendeza pia huja muda mrefu bila kufumua ila unakata sana nywele.

.. Sononeko la mke mwenza, mtindo huu ni maarufu sana uswazi kwa wezi wa mabwana za watu mtasubiri sana. Hapa ni mix grill mabutu kidogo rasta kidogo yani kichwa kizima kinajaa mitindo tofauti.
mtindo wa wagonjwa, wengi husuka hivi wakiwa wanaumwa au wako vibaya na stress kibao.
... Rasta kubwa
.. Rasta ndogo
Zinafanana kabisa na rasta halisi lakni hizi ni za kusuka, wanawake wanaosuka mtindo huu wengi ni wababe, wakorofi, halafu wenye silika za kiume au kutumia mmea
..Mayenu nk nk
Umeupenda upi? Unataka na bei? Unataka na msusi? HAYANIHUSU[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hahahah leo nmesikia hairstyles hata nisizozijua
Tupate na picha bas,
 
Hahahah leo nmesikia hairstyles hata nisizozijua
Tupate na picha bas,
1470507331983.jpg
1470507335686.jpg
 
Haya majina ya mitindo ya nywele hayana tofauti na majina ya mitindo ya nguo uswazi...
 
Back
Top Bottom