Mpenzi Jury

Mpenzi Jury

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
384
Reaction score
658
Miaka miwili iliopita nimekuwa katika mahusiano na mpenzi wangu ambae kwa kiasi nilitokea kumuamini na kujihakikishia kama huyu angeweza kuwa mke wangu hapo baadae,

Mchumba wangu alipata kazi visiwani Zanzibari sikuwa na hiyana bali nilimwambia kwa wakati wote atakapo kuwa Zanzibar tutakuwa tukiwasiliana,

Kila mala alimudu kunipigia simu na mimi nilikuwa nikimpigia simu,

Siku moja aliniambia mazingira ya kazi yake na changamoto alizokuwa akikumbana nazo katika majukumu yake mpenzi wangu aliniambia mme wa bosi wake kuna wakati alimtaka kumfanyia Massage kipindi mkewe alipo kuja bara kibiashara na wakati mwingine akimkumbatia nakumnongoneza masikioni kwa maneno ya mapenzi
Kiukweli mpenzi wangu ni pisi kali ya kwenda kama mjuavyo wana Jamvi wa habeshi wa Manyara kutoka mitaa ya Daleda!

Miss hakuitaji makeups 💄 ili kumvutia kila lijari na mola kamjalia utulivu wa sauti aongeapo huamsha pepo la Ngono hata kama sauti yake imebeba huzuni bado utashutuka kwa maelezo yake,

Kadri tulivyokuwa tukiwasliana na mpenzi wangu ndivyo nilivyo zidi kujenga khofu juu yake na kumuonea wivu wa kimapenzi hasa kwa umbali ulio kuwepo kati yetu,

Nilianza kumtia vishawishi ili arejee na hatimae baada ya miezi kadhaa alinipigia simu siku hiyo huku akinitaka kufika Bandarini ili kumlaki japo nilijua alikuwa akinidanganya lakini alinitumia picha ya Bandari ya Unguja huku akiipanda Azam Marine,

Mpenzi wangu alirejea jijini Dar es salaam"
Nilikuwa nimekaa juu ya sopha huku nikimuangalia Junry alivyo kuwa akiyaandaa mapishi kwa ajiri ya kitoweo chetu cha siku hiyo baada ya kumuasi Muumba,

Junry alikuwa akinielekeza kuwa kesho yake angeelekea kwa wazazi wake mkoani Manyara sababu kilikuwa kimepita kipindi pasina kuonana na Familia yake,

Nilikuwa nikimwitikia sababu nisingeweza kumruhusu kuondoka lakini hata mamlaka yakumzuia sikuwa nayo niliishia kumjengea hoja za kumkatisha tamaa kuhusu hiyo safari yake yakuelekea Manyara,

Siku ya pili aliweza kuondoka nakuelekea Manyara huku tukiwa tumekubaliana aweze kurejea baada ya mwezi mmoja,

Ni kweli muda ulipo fika alinipigia simu huku akiniomba Nauli yakumrejesha Dar es salaam,

Nilituma Nauli kama nilivyotakiwa na mpenzi wangu,

Nikiwa mwenye tumaini moyoni kuhusu mpenzi wangu kurejea simu zake zakawa hazipatikani tena nikajaribu kuwapigia wazazi wake wao wakaniambia kuwa aliondoka Manyara zaidi ya siku mbili,

Sikuweza kumpata katika simu zake moyo ukawa na mashaka juu yake nikamua kumpigia tena mama yake yeye akaniambia kuwa alifika salama Dar es Salaam na yuko Buza Mwanagati huko Temeke,

Nikawa na mashaka juu ya mpenzi wangu ikawaje akayakatisha mahusiano yetu kwa njia ya haraka kiasi hicho,

Ilikuwa ni usiku saa sita nikasikia simu yangu ikiita japo sikuwa na mazoea ya kupokea simu nyakati za usiku nilipo angalia juu ya kioo cha simu lilikuwa jina la mpenzi wangu'

Shauku nikawa na tumaini ili kujua ni kipi angenieleza,

Unanipata Hassan kuanzia leo naomba kila mmoja aendelee na mishe zake na utafute mwanamke mwingine mimi siwezi kuendelea kumkosea Mungu kwa uasherati,

Nimetubu dhambi zangu kwa mtume Mwamposa' na kuanzia sasa nimezaliwa upya hivyo nakuomba utafute msichana mwingine,

Ilikuwa ni taarifa ilio ushitua moyo wangu sababu hatukuwa na ugomvi kati yetu nilibaki nikijiuliza kipi kilicho msibu huyu mwanamke mpaka kufikia uokovu,

Nilijaribu kuwasiliana nae kila mala lakini msimamo wake ulibaki kuwa ni huo na hata nyakati zingine alidiriki kuniambia yeye hafikirii kuwa na mwanaume muislamu maishani mwake,

Nilipiga moyo konde nakukubali maamuzi yake sikujari yalio pita nikazuia mawasiliano nae,

Baada ya miezi mitano kupita tokea tuvunje mahusiano nilijaribu kumtafuta tena ili kumjulia khari,

Hi Juuu!
Mambo vipi?

Hi baby niko powaa"
Nambie?

Mimi sijambo vipi habari za siku"

Ni fresh tu mbona kimia"
Ukaona unisuse kabisa?

Hapana sikutaka kuwa msumbufu!

Wala"

Nammbie mme wangu"

Duh mmeo tena?

Ndio Hassan kiukweli wewe ni mwanaume pekee ulie nipenda kwa dhati ila kwa ujinga wangu nahisi sipaswi kuonana na wewe najihisi mimi ni msaliti,

Kivipi kwani?

Unajua toka tutengane nilipata mwanaume kule mkoani na tulipo fanya mapenzi nikapata ujauzito sasa unakaribia miezi minne na huyo mtu hataki kuwasiliana tena na mimi na nimemshirikisha mama nae kasema hataki hata kuniona"

Hapa ninapo ishi kwa bibi nae anasema hatoweza kunisaidia chochote kutokana na hali ya kipato iliopo hapa Nyumbani sababu mbali na mimi kuna mama mdogo nae kazalia hapa hapa nyumbani na Bwana ake hatoi msaada wowote kwake,

Kazi ya mme wa bibi ni mlizi kwenye magodawn kipato chake ndio kinatusaidia kutupa huduma ya chakula hapa nyumbani,

Nimefikiria kurudi nyumbani lakini kama nilivyo kwambia mama hataki kuniona kabisa na amesema nisisogee nyumbani kwake'

Sijui nitawezaje kuutunza huu ujauzito na kama ningekuwa na uwezo ningeitoa hii mimba!

Jury alikuwa akiongea kwa huzuni sana huku akiyajutia maamuzi yake'

Wakati wote alipokuwa akiongea niliyakumbuka maneno yake yalio jaa ufedhuri na dharau juu yangu nilikumbuka jinsi alivyo nitatiza baada yakunizimia simu nikakumbuka jinsi alivyo niambia mimi muasherati nikakumbuka neno lake la toba"

Nikajisemea moyoni kwa hakika yale Maneno ya Muombee adui yako sasa yalikuwa yakitimia,

Jury alikuwa amepoteza muelekeo baada ya ujauzito na sasa alianza kuiona thamani ya x

Maisha ya mahusiano ni kama kitendawili inawezekana kukitegua ukategua na mguu'

Nikiwa mwenye heri moyoni ndio mwanamke alie nidharau nakuniacha sasa anahitaji msaada wangu huku akiniaminisha kuwa mimi ndio nilie kuwa mwenye mapenzi yakweli ambayo hakuwahi kuyathamini pindi tulipo lala na kuamka pamoja"

Maisha ya jury yamehamia mikononi mwa manani nilitamani kumshauri aende kwa Nabii Mwamposa tena ili akatubu ile toba ya kweli kwa maana alipo kili kutubu hakuwa akimanisha toba ya utakaso wa kiroho ni wazi alitubu kuachana na mimi na kumfata muasherati alie isadikisha dhambi yake ya uzinzi,

Nyakati nikiishi na babu kabla ya kifo chake siku moja alikuwa akitukhadithia maisha yake na mkewe bi Rukia,

Katika simulizi zake alinishika mkono nakuniambia Hassani mjukuu wangu'
Wajue wanawake na misimu yao ya upendo'

Babu akawa akisema'
Mwanamke atakupenda siku mkioana,
Mwanamke atakupenda siku akijua yuko na mimba
Mwanamke atakupenda siku atakapo jifungua mpaka kuachisha ziwa mtoto baada ya hapo upendo hukatika kama msimu wa mvua na kisha mtoto aanzapo masomo mwanamke hujilegeza nakukuteka katika pendo lisilo tamthilika,

Hassan ikitokea mwanao akafaulu masomo yake hapo ndoa yako itakuwa na Amani lakini mtoto asipo fanikiwa kuendelea na masomo mahusiano yako na mkeo yataingia katika migongano sababu hatokuwa na cha kupoteza"

Mtoto akihitimu masomo yake nakupata kazi mkeo atahamia kwa mwanae na wewe utabaki mpweke kwa kipindi kirefu'

Kadri umri wake utakavyo kuwa unaongezeka ataanza kumchukia mwanae na atarejea kwako na hapo mtaanza upya mahusiano yenu ya uzeeni,

Babu akaniambia waheshimu sana wanawake unao ambatana katika maisha yako sababu siku wakitendwa utakuwa wakwanza kukumbukwa na wao,

Ukiona mpenzi wako anakutuhumu jua mapenzi yake kwako yamefika kikomo,

Hasani mjukuu wangu kumbuka kila msimu una Maua yake"

3c1ce839-28f2-4d74-8181-6c43c5be621a.jpeg
 
Back
Top Bottom