Mpenzi wa Harmonize amnunulia saa ya milioni 600

MumbaZ

Senior Member
Joined
Jan 28, 2018
Posts
133
Reaction score
124
Harmonize ameupasua mtandao wa Instagram kwa mshangao baada ya kuweka wazi bei ya zawadi ya saa ya mkononi aliyonunuliwa na mpenzi wake, Sarah.


Kupitia kipande cha video alichoweka akiwa ughaibuni, mwanafamilia huyo wa WCB ameonesha saa aina ya Patek Philippe ambayo kwa mujibu wake imenunuliwa kwa $267,525 (sawa na shilingi milioni 603 za Tanzania).

Mwimbaji huyo ameweka picha ya inayoonesha saa hiyo yenye mng’ao wa ‘ukwasi’ na kuandika, “Put some respect on it, thanks baby @sarah__tz ❤ Google the price.”

Kwa lugha ya nyumbani Tanzania, Hamornize amemshukuru mpenzi wake Sarah kwa zawadi, ametaka anayeiona aipe heshima, lakini pia ametaka udhibitishe kwa kui-google.

Hata hivyo, alienda mbali na kusaidia kuiangalia kwenye Google ambapo ilionesha bei ya $267,525 huku nyingine ambayo ni tofauti na yake ikionesha bei ya $41,479.

Patek Philippe ni saa za adhimu na zenye gharama kubwa, awali bei ya saa zake ilikuwa kati ya $25,000 hadi $300,000. Lakini hivi karibuni, iliibuka saa ambayo ilitikisha soko, gharama yake ikitajwa kuwa $2.5 Million, kwa mujibu wa Business Insider.

Ni Harmonize pekee na Sarah ndio wanaofahamu ukweli wa bei ya saa hiyo. Kama alivyowahi kusema Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, “akili ya mbayuwayu changanya na yako.”
 
Wenye bahati zao kweli wanabahatika na siyo Sisi wengine ambao ukibahatika kupata Zawadi kwa Demu wako basi jua ni ya Gono au Kaswende pekee kama si na ile ya Dally Kimoko.
Na habar za mimba

Akija nayo huku TRA wanamuhusu. Million 600, VAT 18% ni kama m108. Sasa amfahamishe kabisa aliyempa iyo zawadi aje na million 108 mkononi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…