Mpenzi wangu amepoteza mvuto

Mpenzi wangu amepoteza mvuto

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
640
Reaction score
651
Heshima kwenu washikadau

Nina mpenzi wangu ambae tupo kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, huyu binti wakati naanza nae mahusiano alikua na mwili ambao ni standard lakini kwa siku za hivi karibuni amekua tukunyema sababu ya kupenda kufakamia misosi.

Yani huwa haipiti siku bila kunitumia picha za misosi anayokula pindi tunapowasiliana kupitia WhatsApp tena kibaya zaidi ni vile vyakula kunenepesha mwili.

Nimejaribu kumshauri kwamba awe anakula na vyakula vya aina flani ili mwili usifutuke kiasi cha kupoteza mvuto lakini wapi, huwa anasikiliza lakini baada ya siku mbili anarudia yaleyale.

Imefikia hatua mpaka nataka kumuacha mana naona kama anapoelekea itafikia hatua nitashindwa hata kuongozana nae.

Kuna yeyote humu amewahi kutana na changamoto kama hii na je aliitatua vipi katika kunusuru mahusiano?

1622389993842.png
 
Mchane kwamba hupendi alivyofutuka na inaweza kuwa sababu ya wewe kusitisha penzi.
Heshima kwenu washikadau

Nina mpenzi wangu ambae tupo kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, huyu binti wakati naanza nae mahusiano alikua na mwili ambao ni standard lakini kwa siku za hivi karibuni amekua tukunyema sababu ya kupenda kufakamia misosi.
 
Ale kwa kiasi au atakosa mpenzi na pia kukaribisha magonjwa yanayohusiana na unene uliopitiliza.
Uzoefu wangu ni kwamba mtu akishajizoesha kula kula ni kama addiction fulani hua ni ngumu sana kubadilika. Na ubaya wa mwili ukishaongezeka kuja kuupunguza ni shughuli pevu
 
Mwambie ukweli kwamba hupendi maendeleo yake na mwonekano wake wasasa, na mweleze pia kuwa Kama hatopenda kukusikiliza Basi atakuwa anakukosea mno kwamaana hata ikitokea umemuoa Basi hatokusikiliza pia.

Mwambie wazi kabisa kwamba hupendezwi na jinsi alivyo kama hatokusikiliza na kubadilika Basi utam-quit
 
Sema nae huku mwili wako ukimaanisha kinachotoka kinywani mwako..........unene uliopitiliza unapoteza mvuto wa mwanamke na mara nyingi unaambatana na uvivu unaopelekea kuwa mchafu.......


198c7c8231a1046d459cd4171b5a73e5.jpg
 
chai...

Kabla alikuwa mwembamba, sababu hakuwa akifakamia misosi...

Baada ya kuwa naye kawa tukunyema, sababu ni kufakamia misosi...

Kupenda misosi ni tabia, kama ipo sasa basi hata mwanzo ilikuwepo...
 
Amekaa kama Mnaija...

Kuna specie fulani Naija imekaa kama huyu mdada, plus namna amevaa...

She's absolutely gorgeous
Hahaha!!! Inawezekana maana mimi nimeitoa mtandaoni kama kielelezo cha mwanamke ninavyopenda awe.......
 
Mimi nimeshaachana na wanawake wawili kwa sababu hiyo hiyo. Mimi wala sikuwaambia nilichapa lapa kimyakimya
Yaani uliwaacha sababu ya kufutuka tu? Mbona mnatutesa wanaume nyie😒 yaani mnataka tusile tushindie biscuits tu ili tuwe vimbaumbau?
 
Back
Top Bottom