Billie pole kwa yote ambayo unayapitia hususan kwenye msononeko wa moyo unaokunyima amani na furaha kwenye mahusiano yako. Inaelekea mpenzio ni mrembo kwelikweli na ndo linalokunyima raha. Lakini kama yeye mwenyewe kashakuambia usijali inabidi ujikaze kiume na ukubaliane naye na juu ya yote umuamini. na kumuamini huko uanze wewe mwenyewe kujiamini na kubadilisha mindset yako. ukishaweza hii basi wala hutakuwa na tabu. hao wenye pesa na mali nyingi wala wasikubabaishe wanataka tu kumchezea mdada wa watu. lakini pia it all lies with your girlfriend if she really cares and loves you she will stay true to you and not otherwise despite the ukabwela situation you have ingawa siamini kama you are that bad angalau mahitaji muhimu unayamudu.
Jikaze kiume na furahia maisha sio ukae ukisononeka kila siku maisha yenyewe mafupi haya unaweza uka-kanumba (RIP) anaytime anywhere. all the best.