Mpenzi wangu anapenda kutumia lugha ngumu

Mpenzi wangu anapenda kutumia lugha ngumu

Nyamwi255

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2022
Posts
4,848
Reaction score
12,776
Baada ya kujitunza kwa muda mrefu (mashallah),takribani week 3 zilizopita nikampata kijana mmoja tall, handsome, then black (Mungu anajua kumbaa mashallah) baada ya kunitaka kwa kipindi kirefu basi na Mimi nikaamua kum-bless moyo wangu na ye akanibless Wa kwake.

Binafsi nampenda sana na hii ni baada ya yeye kuonesha Kila dalili iliyo nzuri juu yangu.

Lakini tatizo lake ni Moja ana lugha ngumu, yani akiongea na Mimi utadhani anaoengea na msela nwenzake, mara utasikia ananiita majina magumu ukilinganisha na jinsia yangu na status yangu, majina kama jembe, jeshi, kamanda, ndo majina yangu siku hizi, licha ya mm kumuita romantic names ila yy harespond in a good way.

Binafsi sifurahii hali hii hata sjui nifanyeje Kuna muda nawaza ndo ataongea hivi na ba mkwe wake hivi🤔Mfano angalia mazungumzo ya simu baina yetu muda mfupi uliopita

(simu inaita)..
YEYE: Oy oy
MIMI: yes babe nambie
YEYE: kama Kawa?
MIMI: Fresh kabisa
YEYE: Pande zip?
MIMI: Nipo home kwa sasa ila nataka kutoka mara Moja.
YEYE: unaenda wapi?
MIMI:Naelekea ofisini mara Moja nimesahau PC
YEYE: ok, Sema nini mwanangu usikawie kurudi,Nina ubao kinyama, naomba unitolee kitu cha Dona natimba hapo Soon
MIMI: poa usijali
YEYE:Nakubali..

(Nilivorudi nikapika tukala halafu Akala Tena)
Ova.
 
IMG-20240602-WA0303.jpg
 
unajistukia tu huyo ni mwanaume unataka alegeze ulimi kama wewe ?! Unataka ukwambie "niambie mamii" Wewe ni mwanamke yeye ni mwanaume wanaume tuna hulka ngumu kuliko nyie wanawake.
Sema nini msela anakaza sana.
Simaanishi alegeze ulimi ila nkimuita romantic names bas naye arespond vizuri sio kuniita mwamba!
 
Uwezo wa kumbadili unao as long as mnapendana kaa naye kwa ukaribu siku mueleze kipi unapenda na kipi haupendi .

Allah awajaalie mapenzi mema na mkadumu
 
Back
Top Bottom