..Ajira ktk sekta rasmi zimekuwa ngumu sana siku hizi-hata kama umesoma vizuri. Sasa vijana wetu wengi vyuoni hawako realistic, wanakuwa na matumaini makubwa sana ya kupata ajira na "kufanikiwa kimaisha" mara tu baada ya kumaliza chuo. Matokeo yake mtu anatafuta kazi kama miezi 8 hivi bila mafanikio, wakati mwingine miezi inakatika bila hata ya kuitwa angalau kwenye usaili.
Hapo ndipo dada zetu wenye roho nyepesi na wapenda mteremko wa sekenke wanapoanza kutafuta njia za mkato. Njia za mkato sio suluhisho maana hata hao "mabosi njaa" wanajua kwamba ajira ni ngumu na mara nyingi wanakuwa hawana hata mamlaka ya kumuunganishia mtu kazi, leta alone kupendekeza jina lako ili uitwe kwenye interview. Kuna hatari kubwa ya kuliwa kitumbua na kazi usipate.
Pia siku hizi wamejitokeza wajasiriamali wa ajira. NGO inaweka tangazo la kazi na baadaye kukutumia email uende kwenye ofisi zao ambako watakwambia uchangie gharama za kuendesha interview ndipo uitwe kwenye interview. Ikifikia hatua hii, kimbia-hawa ni wajasiriamali tu! Kila la kheri vijana mnaosaka ajira!