Mpenzi wangu haoneshi kumpenda Mtoto wangu

Mpenzi wangu haoneshi kumpenda Mtoto wangu

laolao

New Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
3
Reaction score
15
Nimebahatika kuwa na mtoto na mwanamke niliyekua naye awali lakini hatukuweza kuendelea na mahusiano yale. Mtoto anasoma madarasa ya chini na nmemchukua kukaa naye na kwa sasa nina mwanamke tuna mwaka mmoja pamoja na ambaye tuna matarajio ya kusogea hatua za mbali ikiwemo kufunga ndoa.

Changamoto ninayoipata kwa sasa ni kwamba mpenzi wangu anaonekana kutompenda mtoto, na vitu vingi anafanya kuniridhisha mimi. Anavyoongea naye, anavyomtuma, vitu anavyomwambia afanye ilhali mtoto ana miaka 8 tu vinaniacha njia panda kwamba huyu ni mwanamke sahihi ambaye atamlea mtoto huyu ili apate makuzi mazuri na asi feel ananyanyaswa.

Nahitaji kufanya maamuzi mapema na ikibidi hata kusitisha mahusiano na mwanamke huyu ili mtoto asipate shida mbeleni. Naombeni ushauri kwa wadau mliopitia situation kama hii au kwa mtu mwenye insights/ushauri.
 
Nmebahatika kuwa na mtoto na mwanamke niliyekua naye awali lakini hatukuweza kuendelea na mahusiano yale. Mtoto anasoma madarasa ya chini na nmemchukua kukaa naye na kwa sasa nina mwanamke tuna mwaka mmoja pamoja na ambaye tuna matarajio ya kusogea hatua za mbali ikiwemo kufunga ndoa.
Pole sana mkuuu,

Kwanini mtoto asingekaaa na mama yake na ukawa unamhudumia akiwa kule, kumbuka huyo ni mtoto wa kike na kuna mambo kama ya Binti wa kike angepaswa kumuambia mama yake.

Ingekuwa ni miaka 5 au chini ya hapo ingekuwa sawa lakini kwa huo umri mtoto anaelekea balehe ni vyema angepata malezi ya mama kuweza kujua ABC kuhusu ukuaji wake.

Jaribu angalia tabia za mwanao labda zinamfanya mpenzi wako amtreat the way anatretiwa sasa, may be anakiburi, maneno mabaya, tabia chafu na hamsikilizi mama yake mdogo/mkubwa obvioy hawezi kupendwa.

La mwisho mkumbushe Huyo mwanamke wako kuwa akipenda boga apende na ua lake, huyo binit ni damu yako hivyo anapaswa kumpenda kwasababu ametokana na wewe kama anavyokupenda.

#He/ she who loves u, loves with ur dirty
 
Pole sana na changamoto Single Father.

Aisee, Dalili zimeonekana mapema sana. Ni mbaya.
Unaweza ukazaa na huyo mdada na mkawa na watoto wawili , alaf huyo mkubwa akanyanyapaliwa.

Wako Wamama wanaopenda watoto zao wa Kambo na wanawalea mpaka mtoto anadhan kuwa huyo ndio Mama yake halisi.

Ila kwa huyo wa kwako ni changamoto.
 
Kuishi na mwanaume au mwanamke ambaye ameshazaa na mwanaume au mwanamke mwingine kunaondoa utimilifu wa mahusiano na ladha ya penzi.......

Linajenga doa kwenye mioyo ya wapendanao linalopelekea kila mtu mmoja kuwa na mashaka juu ya mienendo ya mwenzake.....

Hali hiyo ikikomaa huzaa migogoro ya mara kwa mara inayopelekea huzuni na majuto kwenye mahusiano........

Kudate au kuishi na mtu ambaye tayari ana mtoto nje kunataka uwe na uvumilivu wa Hali ya juu na ujasiri wa kipande Cha sabuni kikiwa ndani ya maji......

Word is enough for the wise.......
 
Kumpata mwanamke unayempenda na akapenda mtoto wako huyo pia sio kazi rahisi.

Kumuacha huyo Mwanamke kwasababu hiyo tu pia sio rahisi.

Ukikaa ukiongea nae . Atajitetea na atasema atajirekebisha.
Ila upendo unatoka moyon na hauwez kulazimishwa, ni dhahiri mwanao hapendwi kama unavyotaka ww.

Kumpeleka mtoto kwa Babu na Bibi je?.

Kwa muda kidogo mpaka hapo mnakapo oana na kuwa na familia nyingne alaf ndio uwaunganishe watoto?.

Anyway. Ni changamoto za kifamilia na Kama Baba inabid ucheze karata zako vizur.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ongea naye. Mueleze kama muelewa atakuelewa tu.. ni changamoto sana mtoto/ watoto kulelewa na wa kambo!!
 
Huyo mchumba wako unaishi nae??
Hii hulka imekuja kuwa mbaya sana..

Mwanamke mmekutana tuu mnaanza kuishi hata hajafundwa..hujamuoa anaanza kukupikia kukufulia na umemfanya SOGEA TUISHI.

Hii kasumba imekuwa mbaya sana na mara nyingi wanawake wa hivi huwa ni sawa na mzigo wa mav ukiweza kuubeba utakushinda kwa harufu.

Usifanye mazoea kupita kias kwa mwanamke yaani umtongoze aanze kuja kwako akufanyie kila kitu km mme na mke.kisha aanze kuacha nguo moja moja kila akija hadi mwisho wa siku zijae kabatini kwako kisha kwa uboya wko ukamuoa..nakuhakikishia km una mtoto wako atamuekea sumu amuue ili asimbane mbane.

Mtoa mda km umenielewa chagua moja.
MAKE IT OR BREAK IT
 
Kuna vitu hata huwa havihitaji maelezo mengi na unatakiwa uvielewe kirahisi, naaaa usimlazimishe mtu upendo muache mtu apende mwenyewe....kuku mwenyewe ukimuekea kifaranga sio chake anakifukuza.
Kazi kwako!!!!!
 
Nmebahatika kuwa na mtoto na mwanamke niliyekua naye awali lakini hatukuweza kuendelea na mahusiano yale. Mtoto anasoma madarasa ya chini na nmemchukua kukaa naye na kwa sasa nina mwanamke tuna mwaka mmoja pamoja na ambaye tuna matarajio ya kusogea hatua za mbali ikiwemo kufunga ndoa.

Changamoto ninayoipata kwa sasa ni kwamba mpenzi wangu anaonekana kutompenda mtoto, na vitu vingi anafanya kuniridhisha mimi. Anavyoongea
Ushauri rahisi sana, mwanaume mwenye mtoto aowe mke mwenye mtoto pia, wale watoto wenu wote mtawalea vizuri na kwa amani kabisa.

Hili wala halihitaji rocket science.
 
Kumpata mtu anayekupenda, akampenda mtoto wako na kumhudumia ni bahati sana. Mahusiano ya hivyo yanaanza kuwa magumu just the moment mkianza tu. Bora wote muingie mkiwa moja_moja...au bila_bila.
 
Kuishi na mwanaume au mwanamke ambaye ameshazaa na mwanaume au mwanamke mwingine kunaondoa utimilifu wa mahusiano na ladha ya penzi.......

Linajenga doa kwenye mioyo ya wapendanao linalopelekea kila mtu mmoja kuwa na mashaka juu ya mienendo ya mwenzake.....

Hali hiyo ikikomaa huzaa migogoro ya mara kwa mara inayopelekea huzuni na majuto kwenye mahusiano........

Kudate au kuishi na mtu ambaye tayari ana mtoto nje kunataka uwe na uvumilivu wa Hali ya juu na ujasiri wa kipande Cha sabuni kikiwa ndani ya maji......

Word is enough for the wise.......
You are totally wrong.
 
Ila wanawake wengine bwanaa!hivi unachukia mtoto anahudumiwa na baba yake 100% huyo km mtoto mdogo hampendi baasi ht ndugu hatowapenda..

Mwanao kwanza wanawake wapo tuu!usikubali mwanao anyanyssike kaka..
 
Mama wa kambo huyo kuna wanaoishi na watoto kama wao kuna wanaowanyanyasa,changamoto iko hapo kama umenote tofauti kabla ya ndoa siku ukimuoa ndo utamjua vizuri tena akazaa na watoto wake utajuta kumfahamu,
Yaani kaa ukijua kuna watu wana roho mbaya kiasili hawezi kaa na mtu wa nje ko jipange
 
Ninakushauri kupitia hiki kisa changu...


Miaka fulani , niliwah Date mwanamke mmoja ,Binti tu na uzuri wake.
Yule demu, siku moja,ilikua Jpl. Akaja geto bila taarifa.
Sasa Mimi huwa sipendi kukaa ndani Mwenyewe, Mara nyingi ninaita Watoto wa majirani tunapikaa, tunakulaa, tunaangalia Movies n.k


Sasa yule Manzi , alivyoingia tu Sebuleni Akajichanganya " hivi weee mpuuzi unaiingiza ingiza ndani hivi vipanya vyakooo vinakaaa ovyooovyo , tokeni tokeni panya nyinyi "!
Daahhh aiseee Nilipandwa Hasiraaa. Nilitaka nimchape makofi mazito..


Nikaona huyu nitamuumiza, Basi.. Nikamshika mkono. Nikamtoa nje. Nikamwambia rudi rudi kwako ,!!!
Hakuaminigi kama ndio ulikua Mwisho Wetu !!!.


SIKILIZA..KIASILI MWANAMKE KAUMBIWA HURUMA, UKIONA HANA HURUMA, HUYO ANA ROHO MBAYA, NI MBINAFSI, HAFAI, NA ANAYAFUTA FAIDA YAKE MWENYEWE.
HUYO UKIMZALISHA TU., MTOTO WAKO MKUBWA ATAGEUKA KUA KIJAKAZI.


SASA UFANYE NINI???.

Wewe sio Mimi, Na sijui kina chako cha mapenzi kwake kikoje !!

Hivo, Kaa na huyo Mwanamke, mchane wazi wazi, Bwanaaaeeeh Mimi ndio Baba ,Mtoaji wakila kitu kwenye huu mji, bila shaka wakati nakutongoza ,nilikuambia Nina mtoto, huyu mtoto ni wangu NA LAZIMA umjali kama mtoto wako,.. Mambo unayomtendea huyu Mwanangu ninayaona Mwenyewe kwa macho yangu ,sio kwamba nasimuliwa .


SASA NAKUHITAJI UBADILIKE , KWA MANUFAA CHANYA YA MAHUSIANO YETU.




Asipobadilika, Unaachana naye !!!.
@laolao chukua huu ushauri ufanyie kazi, hakuna mwanamke anapenda mtoto wa kufikia
 
Back
Top Bottom