Mpenzi wangu hataki kuniruhusu niende nje ya Mkoa kiutafutaji

Mpenzi wangu hataki kuniruhusu niende nje ya Mkoa kiutafutaji

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2021
Posts
338
Reaction score
683
Heshima zenu wadau wa jukwaa hili.

Juzi niliandika thread iliyo kwenda na title ya uliwezaje kuachana na mpenzi wako uliye mpenda baada ya kutoa kisa Changu na kusikiliza maoni ya wadau kupitia comment.

Shida yangu ni moja guys, Kuna mishe nataka kwenda kupiga mkoa tofauti na niliopo na kwa mawazo yangu nimepanga Kama Mambo yatakwenda sawa nitaishi huko milele kwakua hapa ninapo ishi ni mkoa wa nyumbani(nilipo zaliwa)na na umenichosha kuishi.

Sasa huyu dem wangu imekua kwake ni ngumu kuniruhusu mm kwenda kutafuta changamoto kwingine, mda wote ananiangaliaa anatoa machozi nikimuuliza sababu ya kulia ana sema wewe unaniacha unaenda mbali kwakwel namuonea huruma nahisi kulia kwake nikama anainajisi safari yangu ya utafutaji.

Pengine kinacho muumiza ni vile tulivyo zoeana tumeishi pamoja lakin biashara niliyo kua naifanya hapa mkoani kwa Sasa ni hasara tupu + kuibiwa ibiwa kwakwel I have to move on kwenye hili, na solution ni kuhama mazingira.

huyu demu nimemuelewesha kwa upana zaid kwanini nataka nihame mkoa kanielewa kishingo upande maana alinambia eti nibaki mkoani nianze kuuza nafaka, (udaga,mahindi,maharagwe) kitu ambacho sijawah kuplan kukifanya.

Kuna wakati nawaza au anachukulia maisha ni simple kwakua nyumbani hua nq hela ya mtaji hata milion 2 na anaziona, au kwakua anapata mahitaji yote kuhimu kwa wakati na hajawahi kulala njaa, na Kama nilivyo sema kwenye thread iliyo pita huyu dem hajui hesabu za fedha yan ukimwambia 10000- 7250 utarudisha chench sh ngap kwa mteja hajui, na HAJAWAHI kufanya biashara yoyote.

Nilicho panga ni hiki.

- Nimeahirisha safari yangu na pesa yangu yote naiweka bank. Kisha namwambia mama, Nimeahirisha kwenda kutafuta kwakua nakupenda na staki nikuumize lakin stotoka popote kwenda kutafuta hela kwakua tumechagua mapenzi kuliko chochote basi acha tufe na njaa ndani ila tuwe wote. Na kwa hili nitakua serious maana naona ananipotezea mda wa kupata MUNGU alicho nipangia kukipata huko niliko panga kwenda.

Mingine guys huyu dem nilimpa nafasi nikamuuliza ikitokea nimeenda dodoma kuishi upo Tayari kuja tuishi wote akakataa, yaaan hataki kutoka mbali na ndugu zake(mama na dada ) baadae akanambia inategemeana Kama kuja kuishi Tena Kama mtu nmpenzi wake siwezi labda mke na mume namie nikakubali ila aniche niende kwanza nikapambane baadae nitamuita.

Lakin kingine akiwa nje na marafiki naona anaongea na kucheka vizuri Sana Kama Hana mawazo, shida akiingia ndani maamaa, anakua Kama mgonjwa mda wote Hana furaha mpaka sio poa.

Wadau USHAURI wenu nifanyeje kwenye hili[emoji19][emoji19].
 
Don't let a stranger decide your future, usiseme haukuambiwa
 
Mkuu hao mademu wa ivo badae wanakuja kukuacha alafu uatajuta nafasi na mda ulopoteza .

Kama unaondoka we nenda tu kama anataka kukusubiri atakusubiri tu kama unaweza nenda nae.
 
Mkuu sjakuelewa vizuri.. Yani unataka kufanya maamuzi juu ya future yako ila unashindwa coz unataka kumplease mwanamke ambae huna mpango wa kumuoa kwa tabia yake ya ulevi?

Akili yako inabidi ipigwe shoti ya umeme ichangamke.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Aisee mmekutana nyote mnafanana akili ama ameisha kusoma kuwa kwake ukwepi kitu.

Hatima ya kesho yako ipo mkononi mwako usiruhusu mtu mwingne akuhamlie kesho yako
 
Mkuu sjakuelewa vizuri.. Yani unataka kufanya maamuzi juu ya future yako ila unashindwa coz unataka kumplease mwanamke ambae huna mpango wa kumuoa kwa tabia yake ya ulevi?

Akili yako inabidi ipigwe shoti ya umeme ichangamke.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] haki anani nahisi kaniloga kabisaaaa.
 
Mbona anakuigizia uyo....? kuwa serious na future yako kumbuka wewe ndiye unaekuja kuangaliwa kama kichwa cha familia apo baadae (tegemezi) sasa kaa apo alafu ghafla bin vuu unashangaa uyo dem kaja kuopolewa na kigogo ndio utajua kua ulikua ujui
 
Back
Top Bottom