Mpenzi wangu kanipa ultimatum kuwa nisipomuoa mwaka huu, atachukua maamuzi magumu

Mpenzi wangu kanipa ultimatum kuwa nisipomuoa mwaka huu, atachukua maamuzi magumu

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Habari za leo watanzania wenzangu?

Nimeshangaa tu jana usiku mpenzi wangu from nowhere kanitumia ujumbe kwenye simu kuwa, mwaka huu ukiisha kama sijamuoa, basi yeye atafanya maamuzi magumu na nisimlaumu kwa lolote.

Hapa nawaza, huyu ni kwamba sasa hivi ana mtu mwingine ndio maana ananipa hii ultimatum au tatizo nini?
 
Miaka mitatu mmehitimu shahada ya nini?

Mahusiano yenye fyucha huwezi kukaa miaka yote hiyo.

Yupo sahihi.
Mahusiano yenye future unatakiwa kukaa muda gani?
 
Mwaka wa tatu huu mkuu
Mkuu unataka ugundue nn kutoka kwake ndio umuoe , maana hiyo miaka ni mingi nahisi umeshajua mapungufu yake na mpaka umekaa kwenye mapenzi muda wote huo ,kila mtu atakua ameyakubali mapaungufu Ya mwenzie , kama unampenda kwa dhani ww muoe tu , changamoto zote watu hutafuta jinsi Ya kukabiliana nazo na c kuzikimbia mkuu
 
Back
Top Bottom