Mpenzi wangu kanipa ultimatum kuwa nisipomuoa mwaka huu, atachukua maamuzi magumu

[emoji16] umegusa mzizi mkubwa saana wa ndoa tulizonazo kwasasa nanyingi zinasua sua saana!! Vijana tujichekeche saana , Ndoa zinakuwa ngumu kutokana na sababu kuu Kama hizi zilizopelekea kufunga Ndoa!!!!

#Umetoa points hizi kama ulikua kwenye brain yangu[emoji120][emoji120]
 
Achana nae, anakuletea kauli za ajabu ajabu. Soko bado liko vizuri, tafuta mwingine songesha mpaka ukiwa tayari kuoa
 
Inabidi iwekwe sheria kabisa mwisho miaka mitatu usipomuoa mmojawapo alipwe pesa
 
Mkuu malengo gan huwez jua huenda malengo yakatima akiwepo yy kina mwanamke na nyota yake hata mm Nina mpango wa kuoa labda maisha yatabadilika nimegundua ukiwa hujaoa matumiz ni makubwa bata mpaka saa nane usiku kwa sabab nan atakuliza ngoja nioe labda tabia itabadilika maana kurud saa mbili home nimeshindwa kabisa
 
Labda ufunguke kwanini hujamwoa huyo bint wa watu au kipi kinacho kuchelewesha mkuu..?
 
Mkuu nakushauri uanze kubadili hiyo mienendo yako kwanza kisha ndio ufunge ndoa.
 
Ana haki ya kukuacha miaka mitatu unataka kugundua nini kutoka kwake?
 
Kama umeridhika na yeye na unaona kabisa she will be a good mother rto your kids muoe tu.

Ndoa raha sana ndugu yangu. Usiangalie ndoa zilizofeli, mbona zipo nyingi tu ambazo watu wamefanikiwa?
 
Mimi nagonga mwaka wa 13 sijaoa bado....
namuahidi nitamuoa 'mke' wangu kwa ndoa ya kidini but tuna watoto watatu
ila mwaka huu lazima nioe
 
Miaka mitatu mmehitimu shahada ya nini?

Mahusiano yenye fyucha huwezi kukaa miaka yote hiyo.

Yupo sahihi.
Mkuu mitatu michache Mimi na minne sasa lkn nilipanga nioe mwaka huu,lkn ntaoa mwakani.
 
Mkuu huo nao ni mtazamo wako siwezi kupinga lakini nizungumzie kdogo swala lako kwamba ukioa utabadilika(umeshindwa kubadilika unasubiri et uoe ndo utabadilika sidhani kama ni sahihi kiivo)ila ni mtazamo wako na naomba mrejesho ukishaoa
 
Ili tuweze kuchangia vizuli tuu Uzi na mleta mada upewe ushauli sahihi mleta mada unatakiwa ufunguke mambo yafuatayo

1.malengo yako na huyu binti ni nini katika mahusiano yenu.

2.je ulishawahi kumuahidi utamuoa ktk mahusiano yenu au

3.kama ndio ulimuahidi utamuoa ni wapi unapokwama hebu tueleze ili tukusaidie jinsi ya kujipanga

4.kama hapana hujawahi kumuahidi kumuoa na huna mipango nae ya kumuoa unataka kukaa na huyo binti ktk hayo mahusiano nae ili iweje mwisho wa siku

5.katika mahusiano yenu ya miaka mitatu nyumbani kwao binti unatambulika

6.Huyu binti ni kweli unampenda au eat and run
 
Miaka mitatu yote unampotezea muda kama huna mpango naye mweleze ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…