Mpenzi wangu kaweka status WhatsApp ya kuachana na mtu ila si mimi

Habari wakuu.

Nimeamka leo nakuta mpenzi wangu kaweka whatsapp wimbo wa Mboso uitwao over akisindikiza na maneno na dhihaka za emoj za kuonesha anamwambia mtu ambae sio mimi.

Kuna haja ya kuhoji?
Tena Bora hajaku mute umeona kabisa mwingine anaku mute huoni kabisa ,kwahyo we kama unampenda tulia husikurupuke
 
Kheri wewe mimi Ali nipigia video call akiwa na jamaa mpya wakaanza kunicheka
 
Usimsemeshe kitu.....ingia status YAKo andika hivi "Asante kwa kuniweka wazi, wako wengi wanaililia hii nafasi, soon nakujibu kwa vitendo".....ukimaliza tulia kimya alafu angalia mienendo yake lazima utagundua kitu na anaweza kujiingiza kwenye mtego mwenyewe.....akikuuliza status Ina maanisha nn, mwambie mambo ya ofisini
 
Sikiliza mkuu hakuna mtu mwenye simu kwa zama hizi mwenye mpenzi mmoja
Narudia tena HAKUNA MTU ANAYEMILIKI SIMU MWENYE MPENZI MMOJA.
 
Uhoji umemuoa? We vunga tu, mwambie hongera kwa kuwapunguzs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…