Mpenzi wangu Ndyoko ndiyo ametumia hizi 'condom' sio mimi!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Hii skendo ilikuwa ni kama 'jumba bovu' mwanaume mkware aliamua kuniangushia mimi
baada ya kuona hakuwa na majibu ya kujitosheleza kwa GF wake baada ya GF wake
kugundua kuwa paketi moja ya condom imetumika ndani ya siku mbili ambazo huyo GF
alikuwa safarini.

Kama kawaida ya wadada, akiwa anafanya usafi ndani ya nyumba akaona kuna mipira 3
kwenye 'dust bin' ikiwa na kile 'kimiminika'. Jinsi GF alivyo makini akaenda kuangalia kwenye
droo ya kitanda kweli akakuta packet moja iko 'empty'. Utata ukaanzia hapo, juu ya nani
katumia hiyo mipira. Ukweli ni kwamba jamaa alileta mwanamke mwingine wakati GF wake
yuko safarini na kuivunja amri ya sita. Sasa lilijisahau kuweka mambo sawa ili kufuta ushahidi.

Sijui niseme jamaa alikuwa na 'akili' au ni ujinga, wazo la haraka lililomjia ni kunisingizia eti
mimi ndyoko ndo nilienda geto kwake kuibanjua amri ya sita na mdada mwingine.
Halfu likaniandikia nimsitiri kutokana na skendo yake hiyo. Na kweli baada tu ya meseji yake kuingia
mara Shemeji huyooooooo, simu inaita. Nilichoamua ni kutoipokea hiyo simu ya shemeji yangu.

Ila nashukuru kwa sasa wameoana na wanaishi kwa amani. Baada ya miaka nane toka skendo hii kutokea
juzi nikakutana nao. Huyo shemeji alivyo na kiherehere, si akaniuliza kuhusu hii maneno......! Nilichomjibu
ni kwamba asahau tu 'UJANA NDO ULIKUWA UNATUSUMBUA".

My take: Jamani vidume tuachanane na mambo ya kusingiziana mambo mabaya. Ukiamua kujitoa muhanga basi uwe tayari kukabiliana na matokeo yake. Hivi kama mimi ningekuwa nimeoa na jinsi ladies walivyo na uchungu wajuapo kuwa mashostito wao wanaibiwa MABF wao, ndoa yangu ingekuwa salama kweli hapo? Nomaaaaa!
 
loh hadithi ya namna hiyo unafikiri wanawake wanaikubali basi? Ila tu wanaamua kupotezea.......aka kufa na tai shingoni
 
Wa siku hizi hatudanganyiki kiurahisi namna hiyo! Yani mtu atoke kwake aje kubanjukia kwa rafiki yake?lodge zote na hotel hajaziona?aisee wajinga ndo waliwao!
 
haiuziki hiyo aise
yaani hapo kwa mke ingekuwa balaa
Hiyo ya kusema rafiki alikuja kwangu wala haina mshiko aise


Konie hujambo
 
ujanja wa kizamani, saiv umdanganye nani namna hiyo! saiv match za nje zinachezwa hukohuko nyumban ni mpenz mmoja tu.
 
Wanawake wajanja na wana hisia kali. we ukiano anataka kukuumbua we jifanye mkali tu.
"yaani wewe unaleta condom zilizo tumia ndani kwangu? leo utanieleza hizo condom ulizitumia na nani. siku zote nakaa humu ndani mbona sijawahi kuziona?". mwendo wa kumgeuzia kibao hadi mwisho.
NOTE:
Usije ukajifanya kuomba msamaha. hawa viumbe hawasamehi wala kusahau mambo yanayo husu mapenzi. wapo radhi wakutoe roho. Mia
 
mkuu upo sawa hata kama ushahidi upo imefanya kosa ni kimlomalia hadi mwisho
 
kuna jamaa aliachiwa box za kondom na mkewe aliyekuwa akienda mkoa kikazi kwa muda mrefu kidogo ili atumie akizidiwa! jamaa akagoma kuzitumia akihofia kuulizwa katumia na nani!
 

sasa naelewa,mbona mwaka huu ntaeleweka,kumbe eh,
 

Mhhhhhh! Mkuu we mwenyeji wa Mara nini!
 
Wa siku hizi hatudanganyiki kiurahisi namna hiyo! Yani mtu atoke kwake aje kubanjukia kwa rafiki yake?lodge zote na hotel hajaziona?aisee wajinga ndo waliwao!
Purple ni nani alikudanganya kwamba Mbekenyela kulikuwa na lodge na hoteli miaka 8 iliyopita?
 
Last edited by a moderator:
I once had the same scenario na gf wangu ila kwangu mie tuliachana mwisho wa siku.
 
Purple ni nani alikudanganya kwamba Mbekenyela kulikuwa na lodge na hoteli miaka 8 iliyopita?

2004 juzi tu hapa hakukua na lodge na hotel??okay kama hazikuwepo huko kwake kulikua kunawaka moto hadi aje kujibanjua kwa rafiki yake na kuacha uchafu??sijui kwa nini wanawake wengine hua wanadanganyika kiurahisi hivyo..kha!
 
Last edited by a moderator:
Ndyoko, huenda kweli ulikuwa uaenda kufanyia matusi kwenye chumba cha rafiki yako ndo maana ikawa ni rahisi kukusingizia. Pia ndo maana hata wewe ukakubali kirahisi ili usipoteze uwanja wa nyumbani
 
Ndyoko, huenda kweli ulikuwa uaenda kufanyia matusi kwenye chumba cha rafiki yako ndo maana ikawa ni rahisi kukusingizia. Pia ndo maana hata wewe ukakubali kirahisi ili usipoteze uwanja wa nyumbani

Kwani si nilishasema mambo ya ujana. Au we umeelewaje, sasa hivi tumeshakuwa vikongwe hii maneno imebaki historia tu, eboo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…