Mpenzi wangu u mzuri

Mpenzi wangu u mzuri

MILL8

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
1,837
Reaction score
879
1. Imelala yoo mwamvuli nitaelezea kdogo kuhusu hilo,umuhimu wake kwangu namsamini sana wala sio muongo na ananijali sana tu.mungu amlinde amweke daima anichunge mimi wake,sitamwacha hata iweje kwan nampenda sana kuliko chochote kilichopo nyumbani kwangu. Nnaishi nae kwangu mm nambalikia kwa kila changu mm mm ni nan hasa kwapendeleo hili nililopata.

2.Nangoja thaman ya mavaz yangu nivaayo kwa mana nimeyapunguza,sherehe yangu sio kuona bali kusikia. wewe walidi mpendwa wangu ninavyo vyumba viwili kwa ajili yako ,kimoja kwaajili ya mapumziko,kimoja kwaajili ya maagano.wewe ni mfano wa konde la mfalme lizaalo maelfu kwa mamia nalo lapendwa zaidi na mfalme ndo jema na la thamani machoni pake. Nalo lalindwa usiku na mchana ili lisiharibiwe kamwe.

3.Maladhi na magugu yaupatayo mmea katika konde huangamizwa
Nao mmea hubaki salama na hushamili kwakua husongwi.ngozi yake hunawili na kuleta tumaini la mavuno mfalme atembeleapo konde hilo, huwasifu wafanyao kaz kwalo kwakua yawapasa

4.Mpenzi wangu mpendwa barua zikufikiazo naliziandika kwa mkono wangu,usistaajabu kwakua ni mimi nami ni wewe wewe ni mimi maana kuujulia mwili wangu uliombali ni jadi.na uumwapo wajitegemeza kwa kua nami ni hoi;ewe mwili wangu kukubuhi kwangu sio kwa mabaya,ila Tamaa yanisonga nayo ni kuu sana.ndugu na jamaa wanambia u kahaba wa mji ,je ,-ewe mwili wangu mwenyewe nisikutumainie? la! Sikia Mimi ni zaidi kwa tumaini kwakua u mimi mpendwa wangu .

5.Macho yangu huangaza na mikono yangu hupapasa ila haishiki ,wewe Huna mfano kwa uzuri mpenzi wangu .upuliziapo utuli huhisi nipo ndani yako,unitazamapo huishiwa nguvu,uongeapo hunituliza,ukwazikapo huniliza,unishikapo huhisi baraka,uingiapo kwangu huhisi nuru .wewe ndio wapekee kwangu. Umebarikiwa wewe Kati ya niwaonao
Umewazidi hakika, hata ukipungukiwa mema ntakuongezea katika yangu ili niende nawe popote.

6.Bwana mungu wangu u funguo wa maisha yangu,umenipa kile kinipendezacho sina shida na wanawake wa mataifa.maana umenipa malkia katika wanawake wote nao wataliimba jina Lake, kwakua kabalikiwa toka kwao ,nae amsogeleae huliwa na makali ya upanga .mimi nimfugaji mwema kwakua kondoo hushiba kandokando yangu na hujilaza kandokando yangu,mpenz wangu utashindwa vipi kunawili kando yangu? wewe ni zaidi ya hua mweupe na wala Huna doa nami hukulinda na kukulisha katika nyumba yangu na vyombo vyangu. Mama yangu hukufumia nguo kila mwaka kwakua u roho yangu, na baba yangu hukupa mwanakondoo kwakua u familia yangu, dada yangu hukufanyia tafrija kwakua u rafikiye.
Vipi kuhusu ndugu zangu wengine.

7.Mwamamke usiye na majivuno mwenye sura ya kuvutia na mdomoni hukutoka maneno yenye hekima na Huna papara mwingi wa busara.mpendelewa na mungu wewe ndio wangu sichoki kukutizama wala kukusikiliza hekima zako,mwanamke usiyefungamana na binti za mataifa u wapekee sana kwangu. Usiye na mawazo ya Mali wala ukuu ,mwenye kujishusha kwa watu wote ewe ndio malkia ufaae kwangu,kwakua wewe u heshima nami ntakupa zawadi ya kuwa mume bora kama ulivo mke bora.maana hilo ndilo la kustahili kwa wema wako.

8.Kwa ndimi zao wenyewe hupaliza sauti zao kwaajili yako nawe ni mkuu sana kwao, miali ya moto iangazayo gizani haikufikii kwa nuru yako u kama jua gizani, mbegu zako hazina mfano kwakua ni bora nazo huzaa sana zipandwapo kondeni .kiango utumiacho kuokea mikate ni zawadi bora toka kwa mama yako kwakua alijua u fundi kwalo,chemichemi unywapo maji ndimi niliifanya kama zawadi kwako nayo imebarikiwa. Tazama ni karibu na pahara upapendapo nami hukaa sana hapo ili kukungoja kama nitakuona karibu yangu ,mpenzi wangu u funguo ya nyumba yangu nataman kuingia ndani yake ,upweke umenisonga nami sili chakula nikipendacho kwakua wewe umbali yangu.
 
Back
Top Bottom