Mpenzi wangu wa zamani anaomba nimchangie kwenye harusi yake

Status
Not open for further replies.
usimchangie, na kwa nini akuombe mchango? anataka kuona feelings zako zikoje...ki ukweli nadhani bado utakuwa unampenda (speaking from experience)...huyo hana lolote anataka kukuumiza....mpotezee
 
usimchangie, na kwa nini akuombe mchango? anataka kuona feelings zako zikoje...ki ukweli nadhani bado utakuwa unampenda (speaking from experience)...huyo hana lolote anataka kukuumiza....mpotezee

kizazi kinachpenda visasi!!!!!!!!!!!!!

yale yanayotokea musoma tunayalaumu, lakini hapa wachangiaji wengi wanasema kwa kuwa alikutenda vile, we mtende hivi.!!!!!!!!!!!!!!!!!! hii ndiyo roho ya visasi........ tunapaswa kuushinda ubaya kwa wema.............. kama takataa kumchangia kwa kuwa alimtenda mambo ya hiyana, basi mpendwa Gender sensitive hatakuwa na haki zaidi ya wale walioua watu 17 wa ukoo mmoja kule musoma kwani wote dhambi yao ni moja, kisasi............... naam, mauaji ni matokeo tu lakini mbegu ni moja, kulipiza kisasi.............. tujihadhari na visasi, tuushinde ubaya kwa wema.....................
 
Msitudanganye bado mnapendana sana na wewe una ka wivu ndio maana hutakikuchanga. Changa tu uwe nae karibu na mwanandoa wake akumaki vizuri siku ya arusi........na baadae aje akutoe meno umenielewa?.
 
Wewe changia tu bana...huwezi jua....anaweza akakupa tena ummege siku akiboreka na huyo mumewe mpya
Nyani ungeweka hivi changia ili siku akiboreka na huyo mke wake basi ye ndo litakuwa chaguo ingawa sitapenda huyu binti arudishe tena majeshi huko ambako alipata majeraha ya moyo.Namshauri tu mie ndo niwe kimbilio lake.
 
Sioni ubaya wa ww kumchangia. Tenda wema uende zako, ni investiment yako katika moyo wake. Huwezi jua ataja kufaa kwa lipi katika mapito ya ulimwengu huu. Shinda hisia na hekima itawale maamuzi yako. Ubarikiwe nawe kumpata wa "kukupa jeuri" ya kuja kuitisha michango kwa wengine siku za usoni.
 

Dada yangu mbona uamuzi ushatoa? Unatafuta ushauri ili iweje?

Au unatafuta vindication?

Kama vipi kata mawasiliano kabisa, maana hizi habari za kuongea ongea zinaweza kuwa zina send mixed signals kwa mwenzako, mpaka anajiona ana uhuru wa kukuomba mchango. Mwambie wewe unaoa sasa, funga vioo, ondoa mzizi wa fitina.

Unless bado una kisebusebu na kiroho papu, sioni tatizo litatoka wapi.

Isije kuwa kesho keshokutwa wamekorofishana ndani ya ndoa ex anajisikia ana nafasi ya kukupigia simu kuanza kukulalamikia, next thing you know anataka kukumbushia.Si mambo hayo. Mark my words.

Kama mngekuwa mmeachana vizuri ningekwambia mchangie, lakini mwenyewe umesema mmeachana vibaya, na umesema umeshamwambia humchangii.

Kama ulitaka vindication hiyo, mimi naona hujafanya vya kutosha, forget kutomchangia, mfungie vioo kabisa hata simu zake usimjibu.

I mean it's not like umezaa naye or anything binding like that, right?
 
kama uli move on na yeye aka move on na bado mnawasiliana kama marafiki wakawaida mchangie tu. na wewe atakuchangie siku yako ikifika.
 
Pia anaweza kumchangia na aisende tu,sidhani hata kama kuna haja ya kuomba ushauri katika hili.......Hasa ukizingatia waliachana kwa amani


Huu ni uamuzi wako kutokana na jinsi unavyoona umuhimu wa kuchangia au kutomchangia, lakini kwa kuwa amekuomba mwenyewe na bado mna mawasiliano ya karibu basi ujue kama hutamchangia atakuuliza kulikoni hukumchangia pamoja na yeye kukuomba kufanya hivyo? Hivyo uwe na jibu tayari pamoja na kuwa haliwezi kumridhisha. Ni vizuri kwamba mliaachana na hamkujenga uadui kati yenu maana maisha yenyewe ni mafupi halafu tena uwe na maadui huku na kule wanaweza kabisa kufupisha zaidi life span yako.
 
As they say, do the needful. Changa kama huna kikwazo cha kiuchumi udumishe udugu
 
Uamuzi uko mikononi mwako!!!Great thoughts umepewa...choose wisely!
 
Sikuhukumu, ila wewe dada unaonekana bado unam-mind jamaa. Achana naye bana. Huna sababu hata ya kuwasiliana naye. nakushauri usimchangie hata thumuni. Ujue pepo wake mwovu anakunyemelea. Ukimwendekeza kidogo tu unajikuta umekuwa mke wa pili au nyumba ndogo yake. Achana naye huyo. Si riziki yako. Usikubali kubembelezwa kama mtoto mchanga kupewa pipi, bazoka, sukari gulu; sijui nini! Kata bomba la mawasiliano ya kawaida, labda bakisha sala tu: mwombee kwa Mungu. Kazi kwako mamaa!
 
Mchangie tuu, hakuna ubaya ukifanya hivyo, ila ujifikirie mara 2 mualiko wa kwenda kusherekea ukija, hilo naona lina utata kidogo, lakini inategemea moyo wako wewe muhusika, kwenda au kutokwenda! kuchanga hakuna neno! changa tuu, hujui ya kesho kutatokea nini au baada ya miaka 10!
 
Nakubaliana na wewe.
Naona wachangiaji wanapuuzia ukweli kwamba mleta mada hayupo comfortable na huyu muoaji kutokana na experience yake mwenyewe, kwamba alicheza na feelings zake na kumuacha kwenye mataa siku ya wapendanao. This guy is an a$$hole, he couldn't find a better day ya ku-break up.

Ningekuwa mie he wouldn't see aint no nickel from me.
 
Ukimchangia au usipomchangia, yote ni sawa. It has to come from the heart. Labda yeye anakutest tu. But to show you are so over him and that he is yesterday's news - mchangie.
 
An eye for an eye makes the whole world blind!
 
Ukimchangia au usipomchangia, yote ni sawa. It has to come from the heart. Labda yeye anakutest tu. But to show you are so over him and that he is yesterday's news - mchangie.

sawa sawa.....mimi GS nakushauri kuwa mchangie...kuchanga ni kufanikisha harusi yake sio lazima uhudhurie...lakini kama alivosema Theodora hapa itaonyesha ukomavu wako.....kwambea upo Next level na hayo yamepita

unless, unatuambia kuwa bado hajatoka moyoni...sasa hivi si una mwingine tayari?

hayo mambo huwa yapo kwa wengi tu lakini kiungwana huwa tunafanya hivyo. so mchangie kadiri ya uwezo wako
 
usimchangie, na kwa nini akuombe mchango? anataka kuona feelings zako zikoje...ki ukweli nadhani bado utakuwa unampenda (speaking from experience)...huyo hana lolote anataka kukuumiza....mpotezee
Personal or shared experience Preta?
 
mpaka umri huu nilofikia, sijawahi kuchangia harusi yoyote na wala sioni faida yake.

na afanikishe harusi kwa pesa yake asikae kuomba watu wamchangie ....usimpe, ndio tunataka kukomesha hii tabia ya michango kwenye harusi...agggr
 
Haina shida kumchangia kiubinadamu si mbaya hata kidogo kutakiana heri katika lile lililo jema
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…