Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,606
- 6,672
Wakuu, taarifa mbaya za sasa ni kuwa mpiga picha wa Gazeti la Mwananchi, Mzee Omary Fungo amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Malawi iliyopo Kiwalani Jijini Dar es Salaam.
Taratibu za Mazishi zinafanyika nyumbani kwake Kiwalani kwa mujibu wa mwanae Juma Fungo wanatarajia kumpumzisha kesho hapo hapo kiwalani tutaendelea kujuzana.
Marehemu mpaka anafikwa na umauti unamkuta alikuwa mpiga picha wa kampuni ya MCL wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti, The Citizen na Mwananchi Digital.
Pia amefanya kazi katika magazeti mbalimbali wakati wa uhai wake.
Pumzika salama Omary Fungo