TANZIA Mpiga picha wa Mwananchi Communications (MCL), Omary Fungo afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672


Wakuu, taarifa mbaya za sasa ni kuwa mpiga picha wa Gazeti la Mwananchi, Mzee Omary Fungo amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Malawi iliyopo Kiwalani Jijini Dar es Salaam.

Taratibu za Mazishi zinafanyika nyumbani kwake Kiwalani kwa mujibu wa mwanae Juma Fungo wanatarajia kumpumzisha kesho hapo hapo kiwalani tutaendelea kujuzana.

Marehemu mpaka anafikwa na umauti unamkuta alikuwa mpiga picha wa kampuni ya MCL wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti, The Citizen na Mwananchi Digital.

Pia amefanya kazi katika magazeti mbalimbali wakati wa uhai wake.

Pumzika salama Omary Fungo
 
Asante, Mh Rais Magufuli, atazikwa na wanandugu............................................. message sent and deliver.
 
Mungu ampumzishe anapopastahili..
 
Kaumaliza mwendo, apumzike kwa amani.
 
Kafa kwa ugonjwa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PKA mzee Omary Fungo! Mungu akujaalie pepoye. Na iwe hivyo.
 
Hii covid-19 hii!
Mungu anaiona lakini.
 
Mbona waandishi wengi walikuwa wanakufa zamani ila mlikuwa hamleti Tanzia? Kwanini sasa hivi ndio mnalazimisha hata receptionist akifa mnaleta Tanzia, why??!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…