OR TAMISEMI
Ministry
- Jul 3, 2024
- 20
- 93
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema maboresho ya Elimu yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita yamechangia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa Halmashauri hiyo hususan ni kwa Shule ya Sekondari ya Mizengo Pinda ambayo imeshika nafasi ya kwanza Kimkoa.
Mhe. Mchengerwa ameyasema Shilingi Bil. 1.2 zililetwa kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambazo zimewezesha kujenga shule 2 za Sekondari mpya katika Halmashauri ya Mpimbwe.
Mhe. Rais zaidi ya hilo katika Halmashauri hii tulileta fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 3, madarasa 10 na matundu ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda, napenda kukufahamisha Mhe. Rais kuwa maboresho hayo yamechangia matokeo mazuri kwa shule hiyo na imeshika nafasi ya kwanza Kimkoa na ina division I na II tu.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati za ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokua akisalimia na wananchi wa Kibaoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi leo tarehe 15.07.2024.
Aidha aliongeza kuwa Halmashauri ya Mpimbwe ilipokea shilingi. Bil. 3.5 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na mpaka sasa imekamila na fedha shilingi Mil 170 kwa ajili ya uboreshaji wa Kituo cha Afya Kibaoni.
Amesema Serikali imeendelea kuimarisha huduma za Elimu, Afya na Miundombinu katika Halmashauri hii na mpaka hivi sasa Halmashauri hii wanapata huduma bora za Afya karibu na makazi yao kupitia vituo vya Kutolea Huduma za Afya vilivyojengwa na kuboreshwa.