PostGE2025 Mpina amjibu Rais Samia: Nilimsikia Mtawala akisema hao wa vyama vingine waliishiwa Pawa. Aliyeishiwa Pawa ni yeye

PostGE2025 Mpina amjibu Rais Samia: Nilimsikia Mtawala akisema hao wa vyama vingine waliishiwa Pawa. Aliyeishiwa Pawa ni yeye

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Aliyekuwa Mgombea Urais 2025 na Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema aliyekuwa nyuma ya vikwazo alivyokutana navyo katika mchakato wa uchaguzi ndiye “aliyeishiwa pawa”, akisisitiza kuwa yeye hajawahi kuogopa mapambano ya aina yoyote.

Mpina amesema alikabiliwa na mapingamizi mawili katika mchakato wa uchaguzi, akieleza kuwa katika pingamizi la kwanza alienda mahakamani na kufanikiwa kushinda kesi hiyo katika Mahakama Kuu.Amedai kuwa pamoja na ushindi huo, alikabiliwa tena na pingamizi jingine, akimtaja Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mmoja wa waliokuwa upande wa pingamizi hilo.

"Nilimsikia mtawala kule Zanzibar akisema eti Lissu na mwenzake Mpiba waliishiwa Pawa, nataka niseme na nirudie tena, aliyeishiwa pawa ni yeye, sijawahi kuogopa mapambano"Akizungumza na Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, leo Agosti 12, 2026, Mpina amesema historia yake ya kukabiliana na changamoto mbalimbali imemjengea ujasiri wa kuendelea na mapambano, akisisitiza kuwa hajawahi kuogopa mazingira yoyote, iwe mchana au usiku.
 
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amemjibu Rais Samia baada ya kudai kuwa Luhaga Mpina na Tundu Lissu, wameishiwa pawa, akisema kauli hiyo si sahihi na kwamba “aliyeishiwa pawa ni yeye.”

Mpina amesema hatua zilizochukuliwa dhidi yake, ikiwamo kuwekwa pingamizi mahakamani ili asishiriki uchaguzi, ni sehemu ya kile alichokiita uoga wa mapambano. Amesema alikabili pingamizi la kwanza na kulishinda Mahakama Kuu, kabla ya kuwekewa pingamizi lingine na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 
Back
Top Bottom