GE2025 Mpina na Mgombea Mwenza wala kiapo Mahakama Kuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
Jana Agosti 25, 2025 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Luhaga Joelson Mpina, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Bi. Fatma Fereji, walifika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria za uchaguzi.

Wagombea hao walikula kiapo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Ndg. Hussein S. Mtembwa, ikiwa ni sehemu ya masharti ya kisheria yanayowataka wagombea wote wa nafasi ya Urais kutimiza sharti hilo kabla ya kuanza rasmi kampeni za uchaguzi mkuu.

​
 
Madalali kazini
 
kila napojaribu kuwaza Sera za Mpina zitakua zipi nakosa jibu, ataongea kipi maana upande wa Pili hautaki kusemwa/kukosolewa kabisa majukwaani na watanzania tumezoea mpizani ili apate popularity lazima asemee mabaya ya CCM na Raisi wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…