GE2025 Mpina na T-Shirt yenye picha ya Magufuli kuomba wananchi wamdhamini ili aweze kugombea Urais. CCM B kazini?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mpina kuvaa picha ya Magufuli wakati wameenda kuomba wananchi wamdhini kama Mgmbea wa Urais ACT inamaanisha nini? Kwamba bado anaamini kwenye uongozi wa Magufuli na chama alichokuwa anakiongoza? Au anakumbuka aina ya uongozi wake ambao ulikuwa unapingwa na wengi ikiwemo hao ACT wenyewe? Au ndio anacheza na akili za Watanzania 'wanyonge' ambao wenyewe wakiona chochote tu chenye jina la Magufuli wanatembea nacho hata kama ni kinyesi?!

Yaani hii imekaaje kaaje wakuu?

====

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo Luhaga Mpina akiwa anaendelea na zoezi la kutafuta udhamini Mkoani Simiyu, leo Agosti 17, 2025 amefika katika kijiji cha Mwanduitinje Wilaya ya Meatu na kuomba udhamini kwa wananchi.

Wananchi katika kijiji hicho wamejitokeza kumdhamini ili aweze kukidhi vigezo vya kuteuliwa kuwania kiti cha Urais.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…