Mpira ni Uchumi, Siasa na Burudani, Rais ameonyesha njia Viongozi wengine, Wadau na Wazalendo tuunge mkono kuhakikisha Simba na Yanga zinashinda

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Kwa sasa mpira ni Biashara kubwa sana Duniani, mpira umekuwa ukichangia kukua kwa Uchumi kwa kutoa ajira, kukuza mitaji na kukuza biashara.

Timu za Simba na Yanga ziko kwenye ushiriki wa ligi za CAF, na hivi karibuni walicheza michezo yao ya kwanza ugenini, hata hivyo hawakufanikiwa kuanza vizuri.

Katika kuhakikisha katika mechi zitakazochezwa mwishoni mwa wiki hii, ambazo wawakilishi hawa wa Tanzania wanacheza nyumbani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kununua kila goli litakalofungwa na timu zetu kwa TZS 5,000,000/= (Milioni Tano).

Lengo la Rais ni kutoa hamasa kwa vijana wetu ili waweze kupata ushindi kwa kuwa kuendelea kushiriki kwa timu hizi katika mashindano haya ni kuendelea kuchochea pia Uchumi wa Tanzania, kuongeza ajira na kukuza mitaji. Lakini pia ni kuendelea kutangaza vivutio mbali mbali vya utalii tulivyo navyo na kuonyesha fursa mbali mbali za kiuchumi tulizonazo na hatimaye kuvutia wawekezaji.

Kwa kuwa lengo la Rais ni jema, lenye tija na manufaa kwa Taifa, ni wakati sahihi Wadau wa mpira bila kujali ni Yanga, Simba, Azam etc, Wafanyabiashara na Wazalendo wote tumuunge mkono Mkuu wetu wa Nchi.

Itapendeza kusikia mzee wetu, Makamu wa Rais - Mpango akitangaza. Tutafurahi kusikia mdau wa mpira na Coacher Mstaafu Waziri Mkuu - Majaliwa akitangaza kununua hata ushindi wa timu zote.

Itapendeza kusikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wabunge wote, Mawaziri wakitangaza kununua ushindi wa timu zote mbili.

Itapendeza kumsikia GSM akinunua ushindi wa Simba na MO akinunua ushindi wa Yanga.

Itapendeza kusikia vyama vyetu vya siasa CCM, CHADEMA, ACT etc vikiweka siasa chini na kuungana kununua ushindi wa timu hizi. Timu hizi zikishinda Watanzania wengi watafurahi, hata nyinyi ni rahisi kutangaza sera zenu kwa watu wenye furaha, mpira unaleta utulivu wa kisiasa pia.

Wadau wengine wa maendeleo, wazalendo na wapenda mpira wote tuweke siasa pembeni tuungane kutoa hamasa kwa kuhakikisha Simba na Yanga zinapata ushindi mkubwa. Kuna wakati ni muhimu Watanzania tukawa wamoja, tukimaliza hili la Kimataifa ndio turudi kwenye ligi yetu ya Usimba, Uyanga etc.

Haijalishi utanunua kwa shingapi au utatoa nini, lengo si ukubwa wa kiasi cha fedha au ukubwa wa kitu unachotoa, lengo ni hamasa kwa vijana wetu waweze kupata ushindi.

Mungu ibariki Yanga na Simba ziweze pata ushindi,
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Mambo ya michezo wakati mwingine sio ya kuingilia kichwa kichwa maana badala ya kuleta hamasa waweza kuleta mtengemano.

Kauli ya Rais yapaswa ielezwe kwa uwazi kuwa kila bao hiyo zawadi ni ya timu nzima sio mfungaji maana inaweza kuleta ubinafsi badala ya umoja katika timu na kukosesha team work.

Niliona Msemaji wa Serikali kama kawaida yake akipitosha nia ya zawadi hii kwa ushamba wake
 
Mambo ya michezo wakati mwingine sio ya kuingilia kichwa kichwa maana badala ya kuleta hamasa waweza kuleta mtengemano...
Yes mkuu Chakaza uko Sahihi kabisa, nafikiri wasaidizi wa Rais wataliangalia na kuliweka vizuri, zawadi zote ziwe kwa timu na sio kwa mfungaji ili kuleta hamasa kwa timu nzima hata kwa goli kipa ambaye nafasi kwake ya kufunga ni kama 0.1%.
 
"mpira ni uchumi,siasa na burudani"naomba ufafanuzi siasa inaingiaje kwenye soka,au soka ina siasa zake?

NB:sibishani nataka nifahamu tu.
 
"mpira ni uchumi,siasa na burudani"naomba ufafanuzi siasa inaingiaje kwenye soka,au soka ina siasa zake?

NB:sibishani nataka nifahamu tu.
Yanga ilitumika hata kwenye kusaidia kupigania Uhuru wa Tanganyika, Mpira unaleta furaha, unaleta umoja na udugu ambayo ndio Maisha ya watu, Siasa ni Maisha ya Watu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…