Mpira, Rushwa na Siasa: Kales Karia wa TFF atakamatwa muda wowote, labda asikanyage Misri

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2019
Posts
2,338
Reaction score
5,271
Kufuatia kukamatwa hapo jana kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bwn. Ahmad Ahmad raia wa Madagascar, kuna kila ishara kuwa watakaofuatia katika kamata kamata hiyo ni Marais wa Mashirikisho ya Soka Tanzania(TFF), Bwana Wales Karia ambaye pia ni mwanachama mkubalifu wa CCM, pamoja na mwenzake wa Cape Verde kwa sababu ni mashahidi muhimu na watuhumiwa wa moja kwa moja wanaotajwa katika kashfa hiyo ya mlungula na kutakatisha fedha - inawezekana hata Waziri Mwakyembe pia akatumbukia mle mle - labda wasikanyage Misri kwenye mashindano ya AFCON.

Bwana Ahmad anatajwa kumwelekeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa CAF Bwn. Amr Fahmy kufanya malipo yasiyo halali ya dola za Marekani 20,000 kwa kila mmoja wa Marais wa Soka wa Tanzania na Cape Verde, Bwn.Fahmy aliamua kutoa taarifa ya suala hilo FIFA na ndipo alipofukuzwa kazi haraka haraka na Bwn.Ahmad.

Sasa mamlaka za kipolisi Ufarasa zimemtia pingu Bwn.Ahmad, wanatafutwa sasa waliopokea mlungula huo wa dola 20,000, Bwn.Wales Karia mwanachama mkubalifu wa CCM, pamoja na mwenzake wa Cape Verde, na wote walionufaika na mgawo huo(seemingly Mawaziri wa Michezo wa nchi husika).

Not long ago watu tulio na akili zetu tulishangaa mno motive ya Bwn.Karia kum-attack wazi wazi Kaka yetu Tundu Lissu kwenye Mkutano usio wa siasa wa TFF, kumbe mwenzetu alijua ana kimeo kinamnyemelea na alianza kupiga yowe hata kabla Polisi hawajagonga mlango wake ili apate msaada wa serikali inayokumbatia mafisadi ya hicho chama chake...Muda ni mwalimu mzuri sana!
 
hapa hachomoki huyu msomali
 
 
Safi sana muda ni mwalimu mzuri sana kila nafsi itaonja mauti.....kama namuona villme Wambura akichekea pembeni. Sasa ajidanganye kupekeka kwato zake Misri kama namwona vile msomali yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…