Mpira ungekuwa unachezwa mdomoni, Mbwiga Mbwiguke wa Clouds FM angekuwa na kiwango cha Messi!

myao wa tunduru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2010
Posts
614
Reaction score
235
Kama kuna mdau yeyote wa soka aliyebahatika kumsikia huyu jamaa katika kipindi cha mchezo redio Clouds bila shaka atakubaliana nami kama jamaa ana kipaji cha kuongea na kama mpira ungekuwa unachezwa mdomoni basi huyu jamaa kiwango chake tungefananisha na kina Messi!

Ningependa tupeane baadhi ya maneno yake anayoyatumia!

Anakuambia yeye fundi wa mpira ukiutaka mpira anakupa kama hataki anakufanyia ubahiri anapiga nje ya kumi na nane mabeki wakizubaa anawafanya kama mahindi machanga hatemi kitu anayatafuna gudugudu!

Huyo ndo Mbwiga baba na mama yake Wazaramo yaani kama sketi na blauzi. Usafiri wa kwenda kijijini kwao uzaramoni anapandia Buguruni stendi siyo Ubungo Bus Terminal!
 
Dah sugu aliwafukuza mbeya!! nimemiss huyo mbwiga.
 
Jamaa aliizungumzia mechi ya Simba na Mfulila Wonderers 'spelling sina uhakika' nikawa kama naiona mechi. Simba alipigwa nne mtungi nyumbani na yeye ugenini akapiga mtu tano kibuyu. Jamaa ni noma.
 
ni wakati gani anasikika?

kipindi hurushwa kila siku jumatau hadi ijumaa kuanzia saa tatu usiku ila mara nyingi mbwiga hupewa karibu na tamati ya kipindi kufanya uzaramo wake!binafsi nakizimika hiki kipindi siku hizi kwa ajili yake kwani jamaa ana vitu vipya masikioni mwangu huwezi pata katika blog yeyote
 
ahahahaha!dah!huyu **** mbwiga mikosi ana maongezi aibu!kama cherehani alivyo fasta
 
Mbwiga ana maneno sana, anakwambia ....sio kubadilikabadilika km sauti ya muuza samaki, akiwa mtaani anauza samaki anabana pua, akirudi nyumbani sauti kibesi, teh!
 
'Anakwambia nr 9 uwanjani anatakiwa awe km gobagoba(I'm not sure)' yaani huko hilo pikipiki sio pikipiki, gari si gari, in short inafanya shughuli zote.
 
jamaa anaujua mpira ule wa kwetu enzi zile tunaruka ukuta tunatua mzunguko halafu unajimwagia maji uanawapa manesi wa red cross mia tatu wanakuvusha kukunawisha unapotelea green stand

tamu sana hizi simulizi

kijiwe
 
Msikilizeni Mbwiga. Nimejaribu kuupload one of the few recordings za mbwiga, I hope itawork. Au mnielekeze ntaziwekaje humu ili nanyi mfaidi.

mkuu imekubali plz endelea kutupia!huyu jamaa namkubali sana hapo nimeisikiliza.....burudaaaniiii!huyu jamaa ana kipaji cha kuongea
 
Namsubiiri leo saa 3 hii ili nimsikie baada mechi ya watani na ukizingatia yeye mbwiga ni mshabiki mkubwa wa simba s c
 

naomba cv yake fasta
 
Msikilizeni Mbwiga. Nimejaribu kuupload one of the few recordings za mbwiga, I hope itawork. Au mnielekeze ntaziwekaje humu ili nanyi mfaidi.

mkuu huna vitu vipya vya mbwiga?au naweza kuvipataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…