Mpira wa Afrika na makocha wa kizungu

Mzee2000

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2009
Posts
528
Reaction score
221
Kwa nini timu za africa zinapenda kuajiri makocha wa kizungu? je mpira wa Afrika utaendeleje kama 'waalimu' wanakodishwa maka nenda mwaka rudi?

Kasumba ya kuwaabudu wazungu haipo kwenye soka tu, hata madini yetu wenyewe lakini tunataka wazungu ndio waje kuchimba, ndio maana wanatudharau sana na kutuona mapunguani.
 
tena ni mizungu iliyochoka, kama hili letu. inachefua sana
 
tena ni mizungu iliyochoka, kama hili letu. inachefua sana

Mkuu Cynic mbona hujafafanua vizuri, lenu lipi manake si yapo matatu ndani ya nchi hii!!!!!
 
Na ndo tutaendelea kuumia kila siku, hawa wazungu sidhani kama wana jipya sana maana miaka nenda rudi wanakuja wanaondoka hakuna lolote la maana, hizo hela zinazotumika kuwalipa tungeanza nazo hata kujenga viwanja japo vya mazoezi huku tukiwatumia makocha wetu kina Kibadeni, Minziro, Jamhuri, Mkwasa na wengine wengi tulionao si afadhali kuliko sahivi mnaleta kocha mgeni gharama kibao halafu timu bado hazifanyi vizuri. Mimi naona hata hawa wachezaji wa kigeni wanaokuja wengine wiki mbili wanaondoka hizo hela zingetumika kuboresha viwanja vya mazoezi vya vilabu ingekuwa ni bora zaidi.
 
Cc Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Cynic mbona hujafafanua vizuri, lenu lipi manake si yapo matatu ndani ya nchi hii!!!!!

Mkuu mkolaj, assessment yangu ni kwamba yote yako sawa tu, hayana mapya (i.e., la stars = la simba = la yanga)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mkolaj, assessment yangu ni kwamba yote yako sawa tu, hayana mapya (i.e., la stars = la simba = la yanga)
Bora hata la Yanga na lile la Simba, hili la stars mimi huwa naliona kama licheza movie la hollywood, ukikuta limepiga ile miwani halina tofauti na John Travota au Steven Seagal.
 
Last edited by a moderator:
Bora hata la Yanga na lile la Simba, hili la stars mimi huwa naliona kama licheza movie la hollywood, ukikuta limepiga ile miwani halina tofauti na John Travota au Steven Seagal.
watu wanalipigia dili lile warudishe hela zao za kampeni
 
Hivi tatizo hasa la soccer la Afrika ni nini?
Makocha wa kizungu? Sera za nchi husika kwenye soccer? Vipaji? Uwekezaji? Uzembe? Gundu?
Tukiwalaumu makocha 'wazungu', kwani kuna sehemu tunalazimishwa kuwaajiri hawa watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…