NDOTO za Yanga kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho la CAF zinaelekea ukingoni baada ya jana Jumanne, Julai 26 kupokea kipigo cha mabao 3-1 ugenini kwa Medeama jijini Accra, Ghana.
Hakuna chochote wanachoweza kukisema kama utetezi wao wakaeleweka na Watanzania, kwa sababu walipata fursa za nyumbani mbili wakashindwa kuzitumia.
Kilichowaponza zaidi Yanga ni ‘utaalamu’ wao wa kucheza na vyombo vya habari – hasa magazetini – na walibweteka mno kwa ‘mpira huo wa magazetini’ kuliko kuandaa mbinu za medani ambazo zingeweza kuwasaidia wakafanya vizuri.
Soma zaidi=>
‘Mpira wa magazetini’ waiponza Yanga, yaambulia patupu Kombe la Shirikisho | Fikra Pevu
Ni kweli lakini ni magazeti ndiyo yanayoitumia YANGA kwa kuuza magazeti hayo...Utaona gazeti linaandika LAZIMA MEDEAMA WAFUNGWE TU, AISEE ....jingine utaona limeandika FOMESHENI YA PLUIJM NI HATARI TUPU...mara kichwa kingine kinasomeka ....YANGA YASAJILI KIUNGO HATARI...Mara gazeti jingine litaandika YANGA IMEPIGA MPIRA MKUBWA...Gazeti jingine linaandika....WALAHI TUNASHINDA...Gazeti jingine utaona limeweka katuni ya Ndege ya kijani angani na kuandika SISI NI WA KIMATAIFA...Gazeti jingine litaandika YANGA, AAAH ACHA BWANA...Gazeti jingine utaona limeandika YANGA TAJIRI mara USAJILI WA YANGA KUFURU TUPU...
Kwa watu wote wenye akili zao yanaychifanya magazeti ya Tanzania ni utoto mtupu...Hivi kuandika YANGA WAPAA KWA NDEGE, ni jambo la kuwaambia watu wazima na akili zao...Hivi kweli kupanda ndege nayo inakuwa issue ya kujivunia?????!!!!!! Mambo haya yangekuwa yanaandikwa na magazeti ya udaku lisingekuwa jambo kubwa lakini mambo haya yanaandikwa na magazeti makubwa ya michezo nchini na kutuacha sisi wengine wengi midomo wazi...
Hivi kweli seriously YANGA ina utajiri gani wa kujivunia???? Utajiri wa mtu mmoja ndiyo unaifanya YANGA ionekane tajiri???? Je, mtu huyo akiondoka YANA itakuwa tajiri???
Magazeti baadala ya kuandika mambo ya msingi na uchambuzi wa kina wa matatizo ya YANGA kiuchezaji yanaandika ushabiki, sijui wale ni WA MCHANGANI, sijui WALE NI VYURA na kadhalika....yaani kinachofanyika ni utoto mtupu....
Hakuna mwandishi makini aliyeandika au kuchambua ubovu wa YANGA kiuchezaji badala yake kinachofanyika (na hata kwa wachambuzi kwenye vituo vyetu vya televisheni) ni kunakiri uchambuzi wa soka ya ulaya na kuuabandika kwenye timu zetu...Utasikia sijui huyu alitoa assist, sijui alipiga kichwa kama mchezaji wa Arsenal...mara mchambuzi utamsikia goli lile lilikuwa ni offside kwa kuangalia marudio ya mchezo au kwa kuonyesha clip ya mchezo mara blah blah blah ....yaani ni uchambuzi wa kitoto kabisa wa 'ku-copy na ku-paste'.
Yaani mimi hawa wadogo zangu waandishi wa habari na wachambuzi wa soka kwenye vituo vya televisheni wananiudhi mno.....kimsingi in my opinion vyombo vyetu vya habari nchini Tanzania ni chanzo kimojawapo cha kuporomoka kwa soka letu...
Kwa mtu makini anayeiangalia YANGA atagundua kuwa YANGA inakabiliwa na tatizo kubwa la mfumo wa uchezaji. YANGA wanaweza kuwa wanacheza mpira wa kupasiana na kumiliki lakini soka hili wanalocheza YANGA halina madhara..YANGA wanapiga pasi za kurudisha nyuma, na kupiga pembeni, na siyo pasi zile za uchonganishi au through balls zinazoweza kuzaa mabao...Ni wachezaji wachache tu wa YANGA wanaoweza kuumiliki vyema mpira pale wanapokabiliana na adui...Yanga wanamiliki vyema mpira pale tu anapokuwa peke yake....wachezaji wa viungo wanshindwa kurudi kwa haraka kusaidia defence pale wanaposhambuliwa...marking ya YANGA ni ya kiwango cha chini mno kama inavyodhihirika na goli lile la kwanza la Medeama jana huko Ghana...Chirwa alikuwa bega kwa bega na mfungaji wa mpira ule wa kona lakini akakata tamaa kumfuatilia mfungaji na hivyo kumwacha aunganishe mpira wa kona na kuwa goli la kwanza...
YANGA ni wabovu katika sehemu nne muhimu: Wanahitaji beki mzuri wa kushoto anayeweza kucheza kwa nguvu na kupeleka mashambulizi na mwenye krosi za hatari. Oscar Joshua ni liability kwani yeye mara nyingi pasi zake ni za kurudisha nyuma, ni mzito kupanda mbele na hata krosi nzuri golini...YANGA inahitaji pia kiungo mkabaji mwenye nguvu ambaye anacheza mbele ya walinzi wawili au watatu wa YANGA...kiungo huyo mkabaji ni lazima awe na nguvu, mrefu, mzuri wa mipira ya vichwa, mkabaji mzuri na anayeweza kumiliki vizuri mpira, kurudi nyuma kusaidia walinzi na kupiga mipira ya nguvu golini kwa adu...YANGA inahitaji fowadi au kiungo mshambualiji mwenye uwezo mkubwa wa umiliki wa mpira, mwenye uwezo wa kutoa pasi na split passes kumfanya Ngoma awe bora...NIYONZIMA hawezi kutoa split passes kwani yeye ana udhaifu wa kutoa pasi za nyuma na za pembeni ambazo hazina madhara...YANGA inahitaji pia mchezaji wa nne ambaye ni winga upande wa kushoto mwenye mbio, chenga, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, mzuri wa mipira ya vichwa na kadhalika.....