Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UWANJA HUU NA MPIRA HUU WA MAKARATASI UNAWEZA KUTOA WACHEZAJI NYOTA?
Nilipenda kucheza mpira toka udogoni na kwa hakika ndiyo mchezo watoto wote mtaani tukiupenda.
Miaka yangu ya utoto nilikulia Moshi Mjini na Mimi na wenzangu tukienda kuangalia mpira mpira King George Memorial Stadium, Lukaranga,
Enzi hizo kulikuwa na timu ya mpira inaitwa TPC kutoka Arusha Chini timu ambayo wachezaji wake takriban wote walikuwa wachezaji wa timu ya Tanganyika katika Gossage Cup ukiwaacha wachache labda wachezaji wawili au watatu.
Nimeleta mukadama huu ili mpenzi msomaji wangu utambua nawazungumza wachezaji wa kiwango gani.
Nimemuona kwa macho yangu Mbwana Abushiri, John Limo, Hemed Seif, Marshed Seif, Emily Kondo, Ishaka Mzee, Awadh Matesa, golikipa Okoth, Dracula, Sembwana, Shariff Salim, Hospitali na wengine wengi.
Hii ilikuwa mwanzoni ya miaka ya 1960 hata muungano bado.
Hawa wachezaji wote hawakupata kucheza mpira wa makaratasi walicheza mpira halisi juu ya kuwa nchi ilikuwa bado Iko nyuma sana inatawaliwa.
Halikadhalika kizazi chetu sisi hatukucheza mpira wa makaratasi.
Mpira wa makaratasi ni uvumbuzi mpya wa miaka hii ya leo.
Picha hiyo ya watoto wawili wanacheza mpira wa makaratasi peku peku tena barabarani si picha ilitakiwa tuwe nayo leo.
Leo ilitakiwa tutazame picha hii kama picha iliyopigwa miaka 100 nyuma iliyopita.
Hii si picha ya leo.
Nakumbuka sisi tulipoacha kucheza mpira nje ya nyumba zetu mitaani hapa Dar es Salaam tunaingia kucheza Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja na Jangwani kwa sisi wa Kariakoo tuliingia katika viwanja hivyo tukiwa tumevaa jezi, bukta na "njumu" kama tulivyopenda kuita viatu vya mpira.
Viatu hivi viwe Gola, Adidas, Puma zote tuliita njumu.
Huwa nikipita mitaani kwetu nakuta watoto wakubwa wanacheza mpira kwenye uwanja ukubwa wake hauzidi wa nyumba ya National Housing Huwa naingiwa na simanzi kubwa.
Nafananisha na utoto wangu miaka 50 iliyopita niko katika uwanja nimevaa jezi, bukta na viatu na stoking na ndani nina "shin guard," hujiuliza kwani kimetokea nini?
Timu ya Tanganyika iliyochukua Kombe la Gossage 1949
Timu ya Tanganyika iliyochukua Gossage Cup 1964
Kushoto: John Limo, Mbwana Abushiri, Hemed Seif na Saleh Zimbwe