Mpira wanaocheza Yanga unatia kichefuchefu

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Yanga na Biashara wamecheza Uwanja wa Taifa kwenye pitch iliyo bora kabisa. Cha ajabu Yanga wameshindwa kabisa kucheza mpira unaoeleweka. Wanabutua butua tu.

Najiuliza hivi afisa uhamasishaji anapata nguvu wapi ya kuwavuta mashabiki waende uwanjani kuisapoti timu mbovu kama hii? Timu imewekeza kwenye mipira ya kurusha kama netball. Sijui kocha anafundisha nini kwenye session ya mazoezi.

Tusidanganyane Yanga ni mbovu, tena mbovu hasaaa! Ni uzembe wa wazi wa Biashara ndiyo ulioipa ushindi Yanga (1:0)

Sidhani kama tarehe 4 mashabiki wa Yanga watajitokeza kwa wingi maana hata sura zao ukiziangalia zimekata tamaa.

Yanga inasikitisha, inakatisha tamaa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Man U hana mpira mzuri na anapigwa na vitimu vidogo ila waulize vigogo wa ligi kilicho wakuta.

Arsenal mpira safiii mbele ya Chelsea kilimkuta nini pia.

Jiandae kisaikolojia mkuu.
 
Hakuna mchezaji wa mikia mwenye mbavu za kurusha mpira. Hivi Gareth Bale hajawahi kurusha mpira kama Bui?
 
Mpira wa Yanga mara ya mwisho kuangalia ilikuwa mwaka juzi nilipoona Yondani kaanzishwa na goalkeeper yeye beki wa mwisho anajaribu kufunga nikaona ni ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema sitaenda,acha kuwasemea watu.......hujalazimishwa kuisupport Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…