Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mpishi maarufu kutoka Uturuki Nusret Gokce amewatia kizunguzungu viongozi wa FIFA kwa kumkuta katika ya uwanja huko LUSAIL siku ya mechi ya finali wiki iliyopita.. Hatimae wakati wa kutangzwa mshindi na kukabidhiwa kombe alionekana akikumbatiana na akina Messi na kulibeba kombe la dunia. Kikawaida kombe hilo huguswa na makapteni wa timu tu na viongozi wa timu pamoja na maraisi wa nchi.
Mbali na mkasa huo wa uwanjani mpishi huyo vile vile aliweka picha hizo kwenye ukurasa wake wa mapishi kwenye instagram