Mpokeeni mdogo wangu huko Uswiss

Jamani kabila ni mtanzania. Atakae kuwa tayari kumpokea wataongea zaidi. Ingawa jaribuni kukumbuka msamaria mwema alimsaidia mtu ambae si wa kabila lake.

Weka jinsia ndugu nikupe kontakiti za mtu wa kumpokea ili kujua jinsi ya kuandaa mapokezi...wa kiume kwa basi wa kike tax...
 
Yeye si wa kwanza. Inapendeza unapokwenda sehemu ukawa na wenyeji, na ingekuwa yeye ni wa kwanza basi uzi huu isingekuwa na maana kwa sababu ingekuwa sawa na kuomba jamvi msibani.

orait orait basi mwache afate taratibu za chuo na za ndege naamini wamampa mwongozo, mengine yatajiseti. Hakuna haja ya publicity
 
Me miaka 30. Jamani lakini mujue issue ni serious

Asante sana ! Nitajitahidi nionane naye, Neuchâtel kule lazima ajue Kifaransa, ...Week end ijayo nitamtembeza kwenye ziwa Neuchâtel na hii summer atafurahi...nidondoshee details za jina na alipofikia
 
Nashukru sana mkuu sasa naanza kupata msaada ninaouhitaji
 
Reactions: Mbu
Asante sana ! Nitajitahidi nionane naye, Neuchâtel kule lazima ajue Kifaransa, ...Week end ijayo nitamtembeza kwenye ziwa Neuchâtel na hii summer atafurahi...nidondoshee details za jina na alipofikia

...LOL...nadhani umuwahishe shopping ya winter warmers kabla pupwe halijaingia....
Mwenzako katokea kwenye Summer ya Bongo, atakushangaa unafurahia jua la nini...
 
Acha wivu bana...ndio yeye ni wa kwanza kwao...kwenye ukoo...kijijini....shuleni kwao/chuoni...ofisini....na pia TANZANIA.Sidhani kama kuna ubaya akimtafutia mdogo wake wenyeji sehemu ambayo hakuwahi kufika kabla...

Si poa jamani, ni kama mnamkejeli badala ya kumsaidia.
 
kazi kweli......naona kwenu huyo ndo wa kwanza kupata mastaz........
 
Si poa jamani, ni kama mnamkejeli badala ya kumsaidia.

"penye wengi kuna mengi,...!"
mtustahmilie tu. Wachangiaji hawana nia mbaya kihivyo,
Dhihaka na vijembe ni sehemu ya mazungumzo...

Naamini hata mwenyewe muanzisha unyuzi huu sasa ameelewa.
Soon mdogo mtu naye apende asipende atakuwa memba wa JF huko Uswizi.
JF ni kijiwe cha wengi waliopo Ughaibuni.
 


Ok mkuu, nimekuelewa vizuri. Na lizzy pia sasa nimemwelewa pia.
 
Hapo nimejibu kwa kifupi jinsi na umri. Umri wangu ni zaidi ya huo.
Nimekusoma sasa...nwy wenyeji wapo ila asiende tu na tabia za ajabu ajabu...na uswahili kama anao auache DIA.
 
Nimekusoma sasa...nwy wenyeji wapo ila asiende tu na tabia za ajabu ajabu...na uswahili kama anao auache DIA.

Mh Spika naomba Mwongozo

1. Mchangiaji amesema tabia za ajabu ajabu ni zipi hizo

2. Uswahili kwanini auachie DIA (nadhani alikuwa ana maana JNIA)

Naomba afute hizi kauli

Naomba kuwakilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…